Mkurugenzi wa Benki Kuu ya
Tanzania Tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa
semina kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT
jijini Arusha Machi 2, 2020.
Meneja Msaidizi wa Uhusiano na
Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina (katikati) akitoa maelezo ya awali
kuhusiana na semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa BoT tawi la Arusha,
Bw. Charles Yamo na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi
BoT, Dkt. Suleiman Misango.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti
za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akitoa mada kuhusu mapitio ya
maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka
2020.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika semina hiyo huku wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa na watoa mada.
………………………………………………
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya
Tanzania Tawi la Arusha Bw. Charles Yamo amewaasa waandishi wa habari za
Uchumi na Biashara kuwa wazalendo kwa taifa wakati wanapofanya
kazi zao
za kiuandishi ili wasije kuibomoa nchi kiuchumi kwa kalamu zao.
Bw. Charles Yamo ameyasema hayo
wakati akifungua semina ya siku tano kwa waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari kuhusu habari za Uchumi na Biashara
iiliyoanza leo kwenye ukumbi wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Arusha.
Amewataka waandishi wa habari kwa
kutumia kalamu zao kutanguliza uzalendo katika kila wanachoandika
kutoka (BoT) kuhusu uchumi na Biashara wahakikishe kinatolewa na Gavana
wa au wasaidizi wake ili wasijeandika habari isiyo na taarifa rasmi na
kupotosha umma wa Watanzania.
“Hakikisheni Mnakuwa Wazalendo
kwa kila mnachokiandika kuhusu BoT ili kulinda uchumi wa nchi kupitia
kalamu zenu mnaweza kubomoa uchumi wa nchi kama msipofuata maadili ya
kitaaluma na kuwa Wazalendo kwa taifa” Amesema Bw. Charles Yamo.
Bw. Yamo amewataka waandishi wa
habari kujiendeleza kielimu na kitaaluma hasa wakibobea katika eneo
fulani badala ya kugusa hapa na pale, hii itawafanya kila mnachoandika
kiwe makini na kisicho na mashaka kwa wasomaji.
“Naomba mkawe makini kusikiliza
kile mtakachoambiwa na watoa mada kuhusu mambo mbalimbali ya Benki Kuu
ya Tanzania BoT ikiwa ni pamoja na Sera ya Fedha, Masoko pamoja na
Mabenki
Katika Ratiba yenu inaonyesha
mtakuwa na ziara ya kutembelea vivutia vya utalii ni jambo zuri. lakini
mimi nawashauri kama itawapendeza mtakapofanya ziara yenu mtembelee
viwanda kwa sababu kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
Rais Dk. John Pombe Magufuli ni Uchumi wa Viwanda, hivyo ingekuwa ni
jambo zuri kama mtatembelea viwanda kadhaa katika jiji la Arusha ili
kuona shughuli za kiuchumi zanavyokwenda.
Benki Kuu inathamini kazi
inayofanywa na waandishi wa habari katika kuwaelemisha wananchi kuhusu
masuala mbalimbali ya uchumi na biashara ndiyo maana tumekuwa tukipata
taarifa mbalimbali kupitia vyombo vyenu vya habari.
Ameongeza kuwa Benki Kuu ya
Tanzania itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kupitia vyombo
hivyo elimu ya shughuli za uchumi na Biashara iawafikie wananchi wengi
zaidi hapa nchini hivyo kuelewa kazi za BoT na kuchochea maendeleo
katika sekta ya fedha nchini.
Amemaliza kwa kuishukuru idara ya
Itifaki na Uhusiano kwa Umma Benki kuu ya Tanzania kwa kuandaa semina
hiyo na kufanyika kwenye tawi la (BoT) jijini Arusha ambalo ni tawi
kongwe sana , tawi hilo ni la kwanza kati ya matawi yote ya (BoT) nchini
na lilianzishwa mwaka 1977.
No comments:
Post a Comment