Pages

Tuesday, March 31, 2020

IGP Sirro Awaonya Watalii Kutojihusisha Na Biashara Ya Dawa Za Kulevya


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu mwingine.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua kituo cha utalii Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kisiwani Zanzibar, huku akiwataka watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kisheria na kufuata maelekezo ya Jeshi hilo.

Kuhusu Corona IGP SIRRO ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kiserikali pamoja na wataalamu wa masuala ya afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis, amesema kuwa, mkoa huo unaidadi kubwa za hoteli za kitalii na kwamba ujenzi wa kituo hicho cha Polisi utasaidia zaidi katika kukabiliana na kuzuia uhalifu.

Ujenzi wa kituo hicho ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 64 zilizotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa utalii visiwani humo.

No comments:

Post a Comment