Pages

Sunday, March 1, 2020

BENKI YA CRDB YAWATAKA AKINAMAMA WAJASIRIAMALI KUCHANGAMKIA FURSA




 Afisa Mahusiano Mwandamizi Wateja Wadogo wa Benki ya CRDB, Seuri Meijo, akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kusaidia wakinamama wajasiriamali wakati wa Kongamano la Mama Lishe lilofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Wakwanza kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole ambaye pia ni mjasiriamali mama lishe. 
Na Mwandishi Wetu
 
Benki ya CRDB imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wakinamama wajasiriamali nchini. Akizungumza katika Kongamano la Mama Lishe lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na Kufunguliwa na Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Seleman Jaffo, Afisa Mahusiano wa Wateja Wadogo wa Benki ya CRDB, Seuri Meijo amesema Benki ya CRDB inachukulia kwa uzito sana suala la kumkomboa mwanamke mjasiriamali kiuchumi kwa kumuwezesha kupitia huduma na bidhaa bunifu.

  Seuri alisema katika kufanikisha azma hiyo Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inabuni fursa za kifedha zinazoleta mafanikio kwa wanawake wajasiriamali wa kada zote.

“Tumefanikiwa kubuni huduma mahsusi kwa ajili ya wakinamama wajasiriamali ukianzia Akaunti ya Malkia, Mikopo ya Vikundi kupitia akaunti ya Niamoja na huduma ya SimAccount lakini pia tunatoa Mikopo ya WAFI na huduma za bima,” alisema Seuri.
Seuri alisema Benki ya CRDB imekuwa ikiwapatia wakinamama wajasiriamali mikopo ya uendeshaji wa biashara na uwekezaji ilikusaidia kupanua biashara zao. “Mpaka sasa tumeweza kutoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 500 kwa wakinamama,” aliongezea Seuri.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo aliipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu wa huduma na bidhaa ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wakinamama wajasiriamli huku akiwataka wajasiriamali hao kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa na Benki ya CRDB kwani zitasiaidia kuboresha biashara zao.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akitoa hotuba yake katika Kongamono la Mama Lishe lililofanyika wilaya ya Kisarawe.

“Tumeambiwa hapa kuna Akaunti ya Malkia inayotusaidia kujiwekea akiba kidogokidogo kila mwezi lakini pia fursa za uboreshwaji wa biashara zetu kupitia mikopo, nawasihi tuzitumie fursa hizi,” alisema Jokate.
Jokate pia aliitaka Benki ya CRDB kusogeza huduma zake kwa wateja kwa kufungua tawi katika wilaya ya Kisarawe, ambapo Afisa Mahusiano Mwanadamizi Kitengo cha Kuwahudumia Wanawake, Rachel Seni alimuahidi kulifanyia kazi ombi hilo huku akimueleza Mheshimiwa Jokate kuwa Benki ya CRDB sasa hivi inatumia zaidi mifumo ya kidijitali kufikisha huduma kwa wateja kama CRDB Wakala, SimBanking na SimAccount ambapo mteja anaweza kufanya miamala yake popote pale alipo.
 Wakinamama wajasiriamali maarufu kama Mama Lishe wakifuatilia kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment