Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe
Luhaga Mpina akikata utepe wakati akizindua jarida la Agribusiness
linalochapishwa na shirika la PASS Trust huku Mtaalamu wa mawasiliano wa
shirika la PASS Bhoke Bevin Mwita akishirikiana naye Kushoto ni
Mkurugenzi wa PASS Trust Nicomed Bohay na kulia ni Mwakilishi wa Baraza
la Kilimo Tanzania (ACT)Bi. Jacqueline Mkindi wakipiga makofi.
Uzinduzi huo umefanyika kando ya
Mkutano wa Tanzania AgriBusness Forum 2020 unaofanyika kwenye Ukumbi wa
Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam ukiwa na kauli mbiu ya
“Kuongeza Tija Kwenye Sekta ya Kilimo na Mifugo Kwa Maendeleo ya
Viwanda”
Jarida hilo lina lengo la kutoa
taarifa zinazihusu kilimo biashara nchini Tanzania likilenga kuwafikia
wadau wakuu katika sekta za umma na binafsi ambapo litachapishwa Mara
mbili kwa mwaka kwa lugha ya kiingereza na kusambazwa kwa wadau.
Mkurugenzi wa PASS Trust Nicomed
Bohay akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe Luhaga Mpina akitoa mada katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.
Mawaziri Innicent Bashungwa
Viwanda na Biashara , Hussein Bashe Kilimo na Luhaga Mpina Mifugo na
Uvuvi wakionesha Jarida la Agribusiness mara baada ya kuzinduliwa kulia
ni Mwakilishi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT)Bi. Jacqueline Mkindi
na Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pass Nicomed Bohay, na mwakilishi wa
Sekta ya Binafsi (TPSF) Bi. Angelina Ngalula.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe Luhaga Mpina akitoa mada katika mkutano huo.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment