Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) Prof Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa BoT leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia Noti
safi. kulia ni Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) na katikati ni Dkt. Bernard Y. Kibesse Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
BoT leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia Noti safi kushoto
ni Bw. Julian Banzi Raphael Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani
………………………………………
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) Florens Luoga amesema benki zote zinapashwa kurudisha pesa zote
chafu benki kuu ya Tanzania ili ziharibiwe na kuingizwa pesa Safi kwenye
mzunguko huku akiwaonya wananchi wanaotumia pesa kinyume na utaratibu
ikiwemo kuziandika maandishi kuwa ni kosa la jinai na watakamatwa na
kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Akitoa Rai hiyo mbele ya
waandishi wa habari habari Gavana wa benki kuu ya Tanzania Florens Luoga
amesema Hadi Sasa benki kuu haijachapisha Wala kuingiza pesa mpya
kwenye mzunguko Tangu mwaka 2009 na kwamba pesa iliyopo kwenye mzunguko
inatosha kabisa kwa mahitaji ya soko.
Benki kuu ya Tanzania inatangaza
Vita kwa watengenezaji wasaambazaji na watumiaji wa Noti bandia huku
ikipanga kuanzisha mkakati maalum wa kuwafundisha wananchi namna ya
kufanya utambuzi wa Noti halali ili kuepukana na utapeli.
Aidha amesema benki kuu
itaendelea kutekeleza Sera yake ya Sarafu Safi huku akiziomba benki zote
kuhakikisha zinatoa huduma rafiki kwa wananchi ili waweze kutumia
mifumo rasmi na kwamba ndani ya saa 24 mteja anatakiwa kupatiwa ufumbuzi
wa matatizo ya kifedha endapo imetokea ikiwa ni dhumuni la kuongeza
haki katika huduma za kibenki.
No comments:
Post a Comment