Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya
utafiti wa kilimo nchini TARI dkr Geofrey Mkamilo ambae pia mratibu wa
kuamasisha upandaji wa michikichi nchini akikabidhi sehemu ya mbegu za
mchikichi zenye uwezo wa kutoa mafuta ya mawese kwa wingi na zinakua kwa
muda mfupi ,mbegu hizo zimekabidhiwa elfu hamsini 50,000 kwa SSP
Dominic Kazimili ambae ndiye mkuu wa gereza la Kwitanga mkoani kigoma
ikiwa njia ya kuteketeza agizo la waziri mkuu katika kupunguza uwagizaji
wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti
wa michikichi TARI Kihinga Dr Philison Kagimbo anaelezea kitaalamu jinsi
ya uzalishaji wa miche ya michikichi ya Tenela yenye uwezo mkubwa
katika utoaji wa mafuta ya kula ambapo moja ya mchakato wake ni pamoja
uwekwa katika pipa na kufukiwa chini na kuwekewa mkaa ili kupata nyuzi
joto 40 kusaidia ukuaji wa miche kwa haraka.
Sehemu ya mbegu 50,000
zilizokabidhiwa na Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kwa gereza la
Kwitanga mkoani Kigoma ,ambapo mbali TARI kukabidhi mbegu katika gereza
hilo pia ameshakabidhi kwa halmashauri sita za mkoa wa kigoma na jeshi
la kujenga taifa JKT Bulombola .
…………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu,Kigoma
Wakulima wa michikichi mkoani
kigoma wamefuraishwa na hatua ya serikali kugawa bule mbegu za muda
mfupi na zenye tija katika ukamuaji wa mafuta ya mawese ya zao la
michikichi aina ya Tenela badala ya mbegu za zamani ambazo utumia zaidi
ya miaka kumi mpaka kuanza uzalishaji.
Wakulima hao wamesema mara baada
ya taasisi ya utafiti wa kilimo nchini TARI kugawa zaidi ya mbegu
50,000 katika jeshi la Magereza Kwitanga kwa lengo la kutekeleza agizo
la serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kuboresha
uzalishaji wa zao la mchikichi ili kupunguza tatizo la kuagiza mafuta ya
kula kutoka nje ya nchi
Akikabidhi mbegu hizo kwa maafisa
wa jeshi la magereza Kwitanga mkurugenzi mkuu wa TARI Dkr Geofrey
Mkamilo amesema wameshaotesha mbegu za kisasa la zao la mchikichiki
zaidi ya milioni 1.2 zenye uwezo wa kutoa mafuta kwa wingi na kuota kwa
muda mfupi ambazo zitagaiwa kwa wakulima na taasisi za serikali bule
na zimesaidia kuokoa zaidi ya bilioni 5.4 ambazo zingetumika kununua
mbegu hizo.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya
utafiti wa kilimo nchini TARI dkr Geofrey Mkamilo ambae ndio mratibu wa
kuamasisha upandaji wa michikichi nchini amesema Tanzania inahitaji
mafuta ya kula tani laki 570 huku yanayozalishwa nchini ni tani laki
205 na kusabaisha kutumia shilingi bilioni 443 kwaajili ya kuagiza tani
laki 365 ili kukidhi hali ya mafuta ya kula hapa nchini.
Ambapo uwoteshaji na Ugawaji wa
miche ya michikichi katika mkoa wa Kigoma kutokana na agizo la waziri
mkuu Kassim Majaliwa unaendelea kwa kasi huku wanatarajia mpaka ifikapo
June 2020 zaidi ya miche milioni 5 itakuwa imeoteshwa kwaajili ya kupewa
wakulima.
No comments:
Post a Comment