Baraka Onyango Raphael (3)ambaye
ana uwezo mkubwa kiakili wa kutaja Marais wa nchi 56 na mawaziri pamoja
na manaibu waziri wa Tanzania bila ya kuangalia popote akiwa na mama
yake Macelina Asango nyumbani kwao kwa mrombo Jana.(Happy Lazaro).
Mfanyabiashara Philemon Mollel
(Monaban)akiwa na mama na mtoto ambaye ameahidi kumsomesha kutokana na
kuwa na kipaji kikubwa kiakili .
*********************************
Happy Lazaro,arusha
Arusha.Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha
Philemon Mollel maarufu kama Monaban amejitolea kumsomesha mtoto mwenye
uwezo mkubwa kiakili aitwaye Baraka Onyango Raphael (3) mkazi wa kwa
mrombo kata ya Muriet jijini Arusha.
Aidha mtoto huyo
ambaye aliwahi kuibuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kutokana na
uwezo mkubwa alionao ikiwemo kutaja mwenyewe idadi ya Marais wa nchi 56
pamoja na mawaziri na manaibu wa Tanzania bila kusoma popote.
Akizungumzia namna
mtoto huyo alivyo na uwezo wa kipekee ,mama wa mtoto huyo Macelina
Asango amesema kuwa,mtoto huyo alianza kuonyesha uwezo huo akiwa na
miaka 2 na nusu,kutokana na wenzake aliokuwa akicheza nao kuona jinsi
ambavyo anaongea mambo makubwa ambayo yaliwashangaza wao.
Amesema kuwa, mtoto
huyo ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia hiyo baada ya
wazazi wake kuona kipaji Cha mtoto huyo ndipo walipoanza kumwuliza
maswali na kushangaa anajibu bila kusoma popote.
“kwa kweli
tunamshukuru Mungu kwa kutupa mtoto huyu kwani ana akili za kipekee sisi
wenyewe tulishangaa Sana anavyowataja Marais wa nchi 56 kwa kichwa bila
hata kusoma popote pamoja na mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya
Tanzania ,baada ya hapo ndipo tulienda kwenye vyombo vya habari na
kuelezea uwezo wa mtoto huyu ili aweze kusaidiwa kielimu kutokana na
uwezo mdogo tulionao wa kumpeleka shule za mchepuo wa kiingireza”amesema
mama.
Ameongeza
kuwa,kutokana na uwezo mkubwa alionao mtoto huyo wanahitaji asome shule
za mchepuo wa kiingireza ili kukuza kipaji chake kwani wao hawana uwezo
wa kumpeleka shule binafsi .
Aidha baada taarifa
za mtoto huyo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ndipo,Mfanyabiashara
Philemon Mollel (Monaban)alipoguswa na kufika nyumbani kwa mtoto huyo
ambaye ameahidi kumsomesha katika shule ya mchepuo wa kiingireza .
Akizungumza wakati
alipomtembelea mtoto huyo,Mollel alisema kuwa,ameguswa Sana na kipaji
alichonacho mtoto huyo na kuwa yupo tayari kumsomesha na atawashirikisha
marafiki zake jambo hilo ili waweze kumsaidia mtoto huyo kufanikisha
ndoto zake.
Mollel amesema
kuwa,mtoto huyo ataanza rasmi shule Januari 6,mwaka huu katika shule ya
mchepuo wa kiingireza ya Pison iliyopo mjini hapa na kwa kuanzia
atamlipia kiasi cha fedha kwa ajili ya kuanzia .
Mwalimu mkuu wa shule
hiyo ya Pison ,Gilbert Sarungi amesema kuwa,wapo tayari kumpokea mtoto
huyo kutokana na uwezo mkubwa alionao wa kutambua mambo mkubwa bila hata
ya kusoma popote.
Amesema kuwa, mtoto
huyo atapewa kipaumbele maalumu kutokana na uwezo mkubwa alionao ambapo
wapo tayari kumpokea Januari 6 shuleni hapo.
Mama wa mtoto
huyo,Macelina ameshukuru Mfanyabiashara huyo kwa moyo wa huruma wa
kumsaidia mtoto huyo ambaye walikuwa wakiwaza namna ya kumpeleka shule
kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake kutokana na uwezo mdogo walionao .
“Nashukuru Sana
jamani vyombo vya habari kwa kunisaidia kumtangaza mtoto huyu na
hatimaye ameweza kupata mfadhili wa kumsomesha shule ya mchepuo wa
kiingireza na nimefarijika Sana kwani ataweza kuendeleza ndoto yake na
kipaji chake cha tofauti alicho nacho”alisema mama wa mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment