Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akimsalimia mzee ambaye hajiwezi
katika Makao ya Wazee Magugu Mkoani Manyara mara baada ya kutembelea
Makao hayo jana kwa lengo la kuongea na wazee waishio katika Makao hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akimsalimia na baadhi ya wazee
wanaotunzwa na kuishi katika Makao ya Wazee Magugu Mkoani Manyara mara
baada ya kutembelea Makao hayo jana kwa lengo la kuongea na wazee
waishio katika Makao hayo.

Baadhi ya Wazee wanaoishi katika
Makao ya Wazee Magugu wakiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Dkt. jana alipotembelea Makao hayo jana kwa lengo la
kuongea na wazee waishio katika Makao hayo.
………………
Na Anthony Ishengoma
Serikali
itaendelea kuboresha na kukarabati miundombinu ya Makao yote ya Wazee
wasiojiweza hapa Nchini kwa lengo la kuhakikisha wazee wote ambao
wamekosa huduma
katika familia na jamii wanaendelea kuishi katika
mazingira bora na salama katika Makao yote yanayomilikiwa na Serikali.
Akiongea na Wazee
wanaoishi katika Makao ya Wazee ya Magugu Mkoani Manyara jana Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
aliwaambia wazee hao kuwa Serikali inafanya ukarabati na kujenga majengo
kwa lengo la kuhakikisha wazee hao wanaishi katika makao yenye staha.
Akiongea na Wazee
Dkt. Jingu aliongeza kuwa pamoja na misaada kutoka kwa wasamalia wema
Serikali inagharimia chakula cha wazee pamoja na kuwapatia huduma za
afya ili kulinda na kuboresha afya zao kwa muda wote wawapo katika makao
hayo yanayomilikiwa na Serikali.
Aidha Dkt. Jingu
aliwataka wazee hao pamoja na wafanyakazi wanaohudumia wazee hao
kuhakikisha wanatunza nyumba za makao ya wazee hao ili nazo ziweze
kuwatunza akiwasisitiza kuahakikisha wanalinda miundombinu yote ya makao
ya wazee.
Dkt. Jingu pia
ameitaka Jamii ya Watanzania kutambua kuwa jukumu la kutunza Wazee sio
la Serikali bali ni jukumu la watoto, na familia ya mzee husika na
kuitaka jamii kuhakikisha inalinda na kuwatunza wazee kwani jukumu la
msingi kwa familia kutunza wazee.
‘’Tunapata maombi
ya kuwatunza wazee kutoka kwa watu ambao kimsingi wana wajibu wa
kuwatunza wazee na kuwambia hapana jukumu la msingi la kutunza wazee ni
la familia’’. Alisisitiza Dkt. Jingu’’.
Dkt. Jingu
alizitaza sifa za mzee anayepaswa kutunzwa katika Makao ya Taifa ya
Wazee kuwa ni yule mzee ambaye kwa namna yoyote ile amekosa ndugu wa
kumtunza na kumlea na hana makazi maalum ya kuishi lakini pia akiwataka
wazee wote wanaoishi katika makao kufuata taratibu za Serikali
zilizowekwa ili kuendelea kuishi katika makao hayo.
Katibu Mkuu Jingu
tayari ametembelea Makao ya Wazee Njilo Mkoani Kilimanjaro na
kuzungumza na wazee wanaoishi katika Makao hayo lakini pia kuangalia
ukarabati wa makao hayo unaoendelea katika Makao hayo yaliyoko katika
Manispaa ya Moshi.
No comments:
Post a Comment