Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha
Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa hafla za
uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya
Bima ya Afya, leo mkoani Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia
Jenerali (Mstf) Emmanuel Maganga akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda wakati
wa hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na
vifurushi vya Bima ya Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga akiongea na wakazi wa Kigoma wakati
wa hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na
vifurushi vya Bima ya Afya, ambapo alisema mnufaika wa vifurushi hivi
atapata huduma kuanzia ngazi ya zahanati mpaka taifa kwa kuzingatia
utaratibu uliowekwa, leo mkoani Kigoma
Mwenyekti wa Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akiongea na
wakazi wa Kigoma wakati wa hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha
wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya, ambapo alisema kuwa
Ukiona mwanasiasa anapinga vifurushi, ujue huyo ni mwanasiasa uchwara,
huyo ni mwanasiasa ambaye haendi hospitali kuona watu wanavyopata shida,
leo mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda, akiongea na wakazi
wa Kigoma wakati wa hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi
kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya ambapo alisema kuwa bila bima
hauna maisha, gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa sana, Bima
inakufanya uwe salama, Bima ni mlinzi kwako na familia yako, leo mkoani
Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia
Jenerali (Mstf) Emmanuel Maganga , akiongea na wakazi wa Kigoma wakati
wa hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na
vifurushi vya Bima ya Afya, ambapo alisema kuwa mpango wa vifurushi vya
bima ya afya ni mfumo bora ambao umejaribiwa duniani unaotumiwa kwa
ajili matibabu na kuwataka viongozi wa Mkoa kwenda nyumba kwa nyumba
kuhakikisha wananchi wanajiunga na mpango huu wa vifurushi
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla za uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia
Jenerali (Mstf) Emmanuel Maganga na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya
pamoja na wakazi wa Kigoma waliokata Bima ya Afya kupitia mfumo wa
Vifurushi.
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
………………
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Wakazi wa Mkoa wa
Kigoma wamesema kuwa mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya ni
mpango
mzuri unaolenga kuwakomboa wananchi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa
huduma za matibabu wakati wowote wanapopatwa na magonjwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakati wa halfa ya uzinduzi wa kampeni ya
kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani
Kigoma , wakati hao wamesema kuwa mpango wa vifurushi unampa mwananchi
fursa ya kuchagua huduma anazotaka kwa gharama nafuuu na kuwa na uhakika
wa kupata matibabu katika mkoa wowote nchini.
Mkazi wa
maeneo ya Mwanga Bw. Nobert Makofi alisema kuwa awali hakuona umuhimu wa
kuwa na Bima ya Afya lakini kwa mpango huu amechukua hatua za kujiunga
na kuahidi kuwa balozi wa uhamasishaji wa wananchi wengine kujiunga na
huduma hiyo.
“Najitolea
kuwa balozi wa kuhamasisha wananchi wenzangu wajiunge, kuna hatari kubwa
ya mwananchi kuishi bila kuwa na uhakika wa kupata matibabu kupitia
bima ya afya, wengi tunapoteza maisha kutokana na kukosa fedha za
kugharamia matibabu lakini mpango huu unatupa fursa kubwa ya kujikinga
afya zetu kwa kujiunga na kifurushi,” alisema Bw. Makofi.
Mwanachama
mwingine Bi. Tausi Kitumbo ambaye amepokea kadi yake wakati wa uzinduzi
ametoa wito kwa akina mama kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii
kujiunga na vifurushi hivyo ili kuhakikisha familia zao zinakuwa na
uhakika wa matibabu wakati wowote.
“Mwanamke
ndio mwangalizi wa familia hivyo kama mama ni vyema ukawa mstari wa
mbele kuhakikisha familia yako unailinda kwa kuikatia kifurushi chochote
na gharama hii inawezekana hata kama kwa kuweka fedha kidogo kidogo,”
alisema Bi. Tausi.
Aidha, Bi
Tausi Saidi amesema kuwa hakuwa amejiunga na mpango wa vifurushi ila
kutokana na hamasa aliyoipata katika uzinduzi wa kampeni hizi
atahakikisha anajiunga na mpango huu kutokana na umuhimu wake kwa afya
yake na anauhakika atakata na kuwa balozi wa mpango huo.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma za Maendeleo ya
Jamii, Mhe. Peter Serukamba alisema kuwa suala la afya sio la mchezo na
ukikutana na mwanasiasa anayefanya upotoshaji kwenye afya huyo ni
mwanasia uchwara na ambaye hatembelei wagonjwa hospitali na kuona
wanavyopata shida.
Akizindua
mpango wa uhamasishaji Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali
Mstaafu, Emmanuel Maganga aliagiza viongozi wote mkoani humo kuhakikisha
wanasimamia suala hilo kwa kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba ili
kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa na wanachukua hatua ya kujiunga.
Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya unaendelea na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mpango
wa vifurushi vipya ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment