Pages

Friday, January 31, 2020

RAIS MAGUFULI ATEUA VIONGOZI WA WIZARA, MAHAKAMA, MAJESHI NA MIKOA


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza majina ya Viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya  Muuungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 31, 2020.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi amewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;
Wizara.
1.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.
2.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu.
3.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Riziki Silas Shemdoe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu.
4.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.
5.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
6.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Leonard R. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala.
Mikoa.
1.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Judica Haikase Omari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga.
2.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Mashauri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
3.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Majeshi.
1.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
2.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) John William Masunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. DCP John William Masunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Ardhi.
1.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Nathaniel Mathew Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Nathaniel Mathew Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
Mahakama.
1.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Wilbert M. Chuma kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
2.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Kelvin D. Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
3.     Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Shamira S. Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
==========
4.     Mhe. Rais Magufuli amewateua Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika, Wakili - Julius Kalolo Bundala na Wakili – Genoveva M. Kato kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hawa itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment