Sehemu ya kikosi cha Mbwa wakiwa
teyari kushiriki kulinda katika mkesha wa mwaka mpya kama walivyokutwa
na kamera ya matukio jijini Arusha leo kabla ya kufanya doria ya ulinzi
katika jiji la Arusha usiku wa mkesha wa mwaka mpya
Sehemu ya Askari wakionyesha
utimamu na utayari kabla ya kuingia mitaani kuhakikisha wananchi
wanasherehekea sikukuu ya mwaka mpya kwa amani na utulivu usiku wa leo
kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha
Askari wa jeshi la polisi mkoani
Arusha wakiendelea na mazoezi ya utayari na utimamu wa mwili kabla ya
kuingia mitaani kuhakikisha wananchi wa jiji la Arusha wanasherehekea
kwa amani na utulivu Sikukuu ya mwaka mpya mazoezi yaliofanyika kwenye
viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo jijini Arusha
Askari wakipanda magari kupita
mitaani kufanya doria kuonyesha utayari na utimamu kabla ya kuingia
mitaani kwenye mkesha wa mwaka mpya jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud
Arusha
…………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la Polisi
mkoa wa Arusha, limesema Arusha sio sehemu salama wala ya kupumzikia
kwa
majambazi,wahalifu na Vibaka bali ni sehemu salama kwa raia wema tu
PIa Kamanda
Jonathan Shana, ametuma salamu kwa Majambazi, wahalifu na Vibaka, kwamba
sumu haionjwi na wakitaka kujaribu basi watainywa halafu watatambua
uzuri wake.
Kamanda Shanna,
ameyasema hayo leo ikiwa ni maandalizi ya kuupokea waka mpya 2020
ambao utaanza rasmi saa 6.00 usiku na kuoengeza kwamba Jeshi la polisi
limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mkesha wa mwaka mpya .
Amesema Jeshi la
polisi litaendelea kufanya kazi ya kuhakikisha usalama na amani ya
kudumu inaendelea kuwepo mkoani Arusha wakati wowote na kuwataka
wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kamanda,Shanna,amesem
Jeshi hilo litaendelea kufanya kazi zake bila kulala wala kupumzika na
limejipanga kuimrisha doria maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu hasa
nyakati za usiku kwenye maadhimisho ya kuupokea mwaka mpya2020.
Kamanda
Shanna,amewahakikishia wananchi wote kwamba Arusha itakuwa shwari
kipindi chote cha siku kuu na baada ya siku kuu na akawaonya Vibaka na
wahalifu wengine kutafuta pa kwenda kwa kuwa Arusha hakuna nafasi hiyo.
Amelipongeza
jeshi la polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kudhibiti matukio
yote ya uhalifu,ujambazi na udokozi kwa kipindi chote cha mwaka mzima
kuanzia January hadi Desemba 31 mwaka 2019.
Amewaambia kuwa
kazi waliyoifanya tangia January mosi mwaka 2019 wanaihitimisha Desemba
31 saa 6.00 usiku na wataanza upya kazi ya ulinzi na usalama kuanzia
saa 6.01 usiku mwaka 2020
No comments:
Post a Comment