Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
maendeleo ya kilimo Tanzania Japhet Justine katikati, akiangalia mahindi
yaliyoletwa katika kiwanda cha Real World Ltd kilichopo Lilambo katika
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma na baadhi ya vyama vya msingi vya
Ushirika wilayani Songea vinavyopata mkopo kutoka Benki hiyo kwa ajili
ya kazi ya kuchakata,kulia Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na
kushoto Meneja wa kiwanda hicho John Mgogo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina
Mndeme kulia akimuonesha jana Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya maendeleo ya
Kilimo Nchini Japhet Justine unga wa mahindi uliochakatwa katika
kiwanda cha Real World Ltd Lilambo mkoani Ruvuma,wakati wa ziara ya
Mkurugenzi wa
Benki ya maendeleo ya kilimo kutembelea vyama vya msingi
vya ushirika vinavyopata mkopo kutoka kwa Benki hiyo ambapo mwaka 2019
TADB ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 2.8 kusaidia vyama sita vya msingi
katika mkoa wa Ruvuma.kushoto meneja wa kiwanda hicho John Mgogo.
Picha na Mpiga PICHA PICHA MAALUM,
*********************************
Na Mwandishi Maalum,
Songea
Songea
BENKI ya maendeleo ya Kilimo
Tanzania(TADB) katika msimu wa kilimo 2019, imetoa zaidi ya shilingi
Bilioni 2.8 kwa vyama sita vya msingi vya Ushirika vyenye wanachama 922
vinavyojihusisha na kilimo cha mahindi mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB
Japhet Justine amesema hayo jana alipokuwa akielezea mikakati ya Benki
hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wakati wa ziara yake
kukagua shughuli za kilimo cha zao hilo zinazofanywa na wanachama wa
vyama vya msingi vya Ushirika mkoani Ruvuma vinavyopata mkopo kutoka
Benki hiyo.
Aidha Justine alisema, Benki ya
maendeleo ya kilimo Tanzania msimu wa kilimo 2020 itaongeza idadi ya
vyama kutoka 6 vya sasa hadi kufikia 18 na imeshatoa bilioni 1.6 kama
mkakati wake wa kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa wakulima wa
mahindi mkoani Ruvuma.
Alisema,huu ni mwaka wa pili kwa
TADB Tanzania kuwapatia mbegu,mbolea pamoja kuwatafutia soko wakulima
wa mahindi ili kuongeza mnyororo wa thamani ambao umewasaidia kuongeza
uzalishaji na kupunguza umaskini katika familia zao.
Kwa mujibu wa Japhet, katika msimu
huu tayari wakulima wa vyama hivyo wameshapata mkopo wa Mbegu na
mbolea kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo wa 2019/2020.
Pia alisema, baada ya kufanya
vizuri katika zao la mahindi Benki hiyo inakusudia kuwafikia wakulima
wa zao la kahawa wa wilaya ya Mbinga ili nao waweze kunufaika na Benki
hiyo ambayo ni kiungo muhimu kwa wakulima na taasisi nyingine za fedha.
Alisema mbali na kusaidia
kuongeza mnyororo wa thamani kwenye zao la mahindi, TADB
inawaunganisha wenye viwanda na wakulima kwa ajili ya kupata bidhaa
jambo lililo saidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuondoa tatizo
la soko la mahindi kwa wakulima.
Ametoa wito kwa wafanya biashara
mkoani Ruvuma ,kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanzisha viwanda vya
kuchakata mazao na Benki hiyo iko tayari kushirikiana nao kwa kutoa
ushauri na mitaji kwa kushirikiana na Benki nyingine zilizopo hapa
nchini.
Aidha,ameipongeza Serikali ya mkoa
wa Ruvuma kutokana na juhudi kubwa inazofanya ya kushauri na kusimamia
suala zima la kilimo, na kuufanya mkoa huo kuongoza kwa uzalishaji wa
mazao ya chakula na biasahara hapa Nchini.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina
Mndeme ameishukuru Benki ya maendeleo ya kilimo kwa kazi nzuri
inayofanya kusaidia mnyororo wa thamani kwa zao la mahindi jambo
lililosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao kutoka tani milioni 1.4 mwaka
2018 hadi kufikia tani milioni 1.6 mwaka 2019.
Alisema, Serikali ya mkoa
itaendelea kuwasaidia wakulima kwa ushauri ili waweze kuongeza
uzalishaji wa mazao ili kuinua hali zao za maisha, ambapo ameiomba
Benki hiyo kufungua tawi lake mkoani hapa ili wakulima wengi waweze
kufikiwa kwa karibu na huduma zake na Serikali ya mkoa itatoa
ushirikiano katika mchakato mzima wa uanzishwaji wake ikiwemo kutoa
ofisi.
Alisema, asilimia 96 ya wakazi wa
mkoa wa Ruvuma ni wakulima na wanategemea sana kuendesha maisha yao
kupitia shughuli za kilimo,kwa hiyo mkoa huo unahitaji sana Benki ya
TADB kuwaunga mkono kwa hali na mali ili waendelee kuzalisha.
Mndeme, ameiomba Benki ya
maendeleo ya kilimo Tanzania kuuangalia mkoa huo kwa jicho la huruma
kutokana na kazi nzuri inayofanya katika uzalishaji wa zao la mahindi
na mazao mengine kama mbaazi,ufuta,korosho,soya,maharage kwa TADB
kufungua tawi ili kusaidia shughuli za kilimo.
Mkuu wa mkoa alibainisha
kuwa,kipaumbele cha mkoa huo ni uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza
thamani ya mazao ya kilimo na samaki ambao wanapatikana kwa wingi katika
ziwa nyasa ambapo mwaka 2019 mkoa ulitenga hekta milioni 1.6 kati ya
hekta milioni 3.3 zinazofaa kwa shughuli za kilimo.
Pia Mndeme ameiomba Benki hiyo
kusaidia kufufua kiwanda cha kusindika zao maarufu la Tumbaku kwani kama
kitarudi katika hali yake na kufanya kazi, zao la Tumbaku litapata soko
la uhakika sambamba na kutoa ajira kwa watu wapatao 350 na hivyo kuinua
maisha ya wananchi na uchumi wa mkoa huo.
Mmoja wa watu walinufaika na mkopo
wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania John Mgogo anayemiliki kiwanda
cha Real World Ltd kinachozalisha bidhaa za Ample ameishukuru Benki
hiyo kwani imesaidia sana kutimiza yake ya kumiliki kiwanda.
Alisema, kwa sasa kiwanda hicho kinachakata chakula cha mifugo kama kuku,nguruwe na samaki na kina uwezo wa kuzalisha tani kumi kwa siku.
Alisema, kwa sasa kiwanda hicho kinachakata chakula cha mifugo kama kuku,nguruwe na samaki na kina uwezo wa kuzalisha tani kumi kwa siku.
No comments:
Post a Comment