
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Vijana Zanzibar Wakiskiliza ajenda za kikao cha Baraza la Watendaji la
Vijana robo ya pili, wa pili (Kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Taifa Khamis Rashid Kheri Kikao kilichofanyika Ofisi ya Vijana huko
Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B”.
Mjumbe wa Baraza la Vijana
Zanzibar Kheri Hassan akichangia Baadhi ya Ajenda zilizowasilishwa
katika Kikao cha Baraza la Watendaji la Vijana robo ya pili huko Ofisi
ya Vijana Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B”.

Mjumbe wa Baraza la Vijana kutoka
Pemba Mwinyi hamadi Othman akielezea juu ya kuhamasisha Vijana wa Pemba
kujiunga na Mabaraza ya Vijana huko Ofisi za Baraza hilo Mwanakwerekwe
Mjini Zanzibar.
……………….
Na Kijakazi Abdalla,Maelezo
Kuanzishwa kwa
Mabaraza ya Vijana Zanzibar kumewawezesha vijana kupiga hatua
mbalimbali
ambayo inayomuezesha kijana kuweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.
Hayo ameyasema
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Zanzibar Mwanaidi Mohd Ali katika kikao
cha robo ya pili kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa Baraza la
Utamaduni Mwanakwerekwe.
Amesema
kuanzishwa kwa mabaraza ya vijana kumewezesha vijana kuimarisha kwa
kutoa maamuzi ambayo yameweza kufikia malengo ya kuwapatia maendeleo
katika Nyanja tofauti.
Aidha amesema
kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuona vijana wanaweza
kujikomboa katika maisha hasa ikiwemo suala la kiuchumi,kijamii na
kisiasa.
Vilevile
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mabaraza ya vijana yamekuwa na fursa
mbalimbali zikiwemo kupata mafunzo ya ufundi na miradi ya kimaendeleo
ambayo imekuwa ikizisaidia vijana katika kujikwamua kimaisha.
Nae Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheri amesema Serikali kupitia
mabaraza ya vijana kumewezesha kusimamia vijana 150 kwa kila Wilaya
kuweza kuwapatia mafunzo ya ufundi ili kuweza kukabiliana na maisha ya
kila siku.
Aidha amesema
katika kuona vijana wameweza kuwa na maamuzi sahihi ambayo yamewezesha
vijana kuingia katika fursa za kugombania uongozi ili kutekeleza
demokrasia.
Nae Mjumbe wa
Baraza la Watendaji Taifa Pemba Mwinyi Hamad Othman amesema mabaraza ya
vijana yamekuwa na mchango mkubwa kwa vijana kwa taifa kwani vijana
wengi wameweza kujiajiri kupitia miradi ya mabaraza.
No comments:
Post a Comment