***********************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Mkurugenzi mtendaji Wa kampuni ya L-VIC
investments limited Bw. Anic Kashasha amesema kuwa kagera ina fursa
nyingi za kutosha lakini kampuni hiyo imekuja na mpango Wa Lake Victoria
Basin Tourism Expo ambapo mpango huo utajadili mnyororo Wa thamani
katika fursa hiyo ya utalii.
Akizungumza na waandishi Wa habari Bw. Kashasha
amesema kuwa wanakagera sasa hasa wale wanautalii wadogo watanufaika
zaidi ikiwa mpango huo Wa Lake Victoria Basin Tourism Expo utajadiliwa
katika kongamano litakalofanyika katika ukumbi Wa ELCT Bukoba ikiwa
lengo ni kujadili mnyororo Wa thamani kuhusu utalii pamoja na hifadhi
za taifa ambazo zimezinduliwa katika wilaya ya karagwe na kyerwa.
“Niseme tu kuwa wanakagera wachangamkie fursa
zinazokuja kutokana na kupata hifadhi tatu za utalii kama burigi
chato,Ibanda Kyerwa, na Rumanyika karagwe ambapo katika kungamano hili
wawasilishaji Wa mada watakuwa ni tanapa lakini pia niseme kutakuwepo
mada mbalimbali zinazohusu utalii” alisrma bw. Kashasha.
Hata hivyo amaeongeza kuwa kutakuwepo na
wahusika wengi pamoja na wafanyabiashara hata waandaji Wa safari za
utalii Wa utamaduni lakini pia watu Wa CRDB kagera watakuwepo mamlaka
ya mapato Tanzania pamoja na shirika la ndege ATCL zikiwemo na taasisi
mbalimbali za serikali.
Sambamba na hayo amesema kuwa kampuni hiyo
ilikuwa na mpango wa kuanzisha fursa ya utalii ya Lake Victoria Basin
Tourism Expo ndani ya miaka zaidi ya mitano ambapo lengo kubwa zaidi ni
kujadili fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya utalii kagera
na kuwataka wananchi pamoja na wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo.
ReplyForward
|
No comments:
Post a Comment