Moja
ya mabwawa ya maji yaliyoharibika wilayani Handeni na kupelekea
wananchi kukosa huduma ya maji kutokana na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha
na kusababisha mafuriko
WAZIRI
wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella wakioangalia maeneo mbalimbali ya mabwawa hayo ambayo
yameathirika
WAZIRI
wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya
ya Handeni Godwin Gondwe kulia katikati ni Mbunge wa Jimbo la Handeni
mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella aliyevaa kofia na miwani
WAZIRI
wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akiwa na Mbunge wa Jimbo la
Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Handeni William Makufwe
WAZIRI
wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akisisitiza jambo kwa Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembela
eneo la mabwawa hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni (CCM) Omari
Kigoda
muonekano wa moja ya mabwawa ya maji wilayani Handeni
WAZIRI
wa Maji Pro,Makame Mbarawa amelazimika kufanya ziara ya wilayani
Handeni Mkoani Tanga ili kuona namna ya kuweza kuwanusuru zaidi wananchi
elfu 55 waliokumbwa na tatizo la kukosa huduma ya maji safi na salama
kutokana na mabwawa 12 yaliyokuwa yakitumika kutoa huduma hiyo
kuathirikawa na mvua zilizonyesha Mkoani hapa.
Mvua
hizo ambazo zilisababisha athari kubwa ya kusomba mabwawa hayo ya maji
na kupelekea wananchi hao kukosa maji wilayani humo jambo lililomlazimu
Waziri huyo kuambatana na viongozi Mamlaka mbalimbali za maji ili kuweza
kurudisha huduma hiyo na kuwanasuru wananchi hao na ukata wa maji.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea mabwawa hayo yaliyobomolewa na na mvua hizo,
Waziri Mbarawa alisema kwamba hilo ni janga ambalo linaweza kutokea
wakati wowote hivyo kupitia Mamlaka zilizopo watahakikisha mji huo
unapata maji kwa kuunganisha na mradi wa maji wa htm Korogwe ambao
utaleta maji Handeni ambapo kunatakiwa bomba la mita 300 wataalamu
wataletwa ili kuweza kufanikisha suala hilo.
“Leo
Bomba litafika kwa sababu kuna miradi mingi inaendelea kwenye mamlaka
zote nchini watatoa bomba haraka lije hapa na tuna timu ya wataalamu
kutoka mikoa ya Moruwasa, Tanga Uwasa na Dawasa lakini bomba likifika
haraka lifungwe kuondosha changamoto hiyo haraka “Alisema
Waziri
Mbarawa alisema kwamba wataalamu wanapaswa kufanya kazi kwa kipindi cha
wiki moja ili huduma ya maji iweze kujerejea Wilayani hapa huku maeneo
ya vijiji yaliyoathirika wataalamu wa bonde la mto Pangani wanatakiwa
kuchimba visima harakaharaka na kwa kutumia gari lililopo Wilayani
Pangani namba 83 kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
“Tunachokifanya
hapa ni jambo la dharura hawa watu watakao kuwa na shughuli za
uchimbaji wa visima natambua watu wa Tanga-Uwasa wapo hapa mtawapatia
fedha kwa ajili ya shughuli hiyo na ianze mapema iwezekanavyo”Alisema
Prof,Mbarawa.
Akizungumzia
mipango ya muda mrefu alisema ili kuondoa tatizo hilo watahakikisha
wanaona namna ya kujenga miundombinu imara ikiwemo kuongeza nguvu kwa
lengo la kuweza kuyaangalia upya mabwawa yote yanakuwa salama zaidi ili
zinaponyesha mvua zisiweze kuleta athari kama iliyojitokeza na kupelekea
wananchi kukosa huduma hiyo muhimu.
“Lakini
pia tutahakikisha tunayalinda mabwawa hayo kwasababu bwawa ni jambo
kubwa sana na kama tusipifanya hivyo yanaweza kupasuka na kuleta athari
kwa wananchi pia tutaangalia mipango yake ya kupitia na sisi wizara
tutaongeza nguvu na utaratibu mpya kuweka ulinzi kwenye sehemu ya
mipango yake ya kupitia kama yanaweza kupita na yanakuwa salama na
wananchi waweze kuepukana na athari”Alisema
Akieleza
namna walivyopambana na suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella alisema baada ya kuwepo kwa tatizo hilo alikutana na Meneja wa
Ruwasa Mkoa ambaye alieleza namna alivyoandika mapendekezo yake na na
kuyawasilisha wizarani ambpo waziri huyo ulimuelekeza Naibu Kati bu Mkuu
ufike eneo hilo na aweze kujionea hali halisi.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kwamba jambo hilo liliwapa faraja kubwa kutokana
na kwamba serikali kuwakimbia wakati wa tatizo hilo ambalo lilikuwa
limeshawavuka uwezo wao lakini kwa ujio wake wanamatuimani wanaweza
kupata ufumbuzi wa mji huo kupata maji ya kutosha.
“Ninaishukuru
wizara imefanya jambo kubwa muhimu kufanya kuhakikisha Handeni inapata
maji ya kutosha ambayo miaka ya nyuma haikuwahi kupata na changamoto
hiyo imepeleka kubomoka madaraja na barabara kwa maana presha ya maji
ikawa kubwa hivyo niishukuru sana “Alisema RC Shigella.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment