Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akitembelea jengo la Mahakama Kuu
Kanda ya Mbeya leo. Kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mbeya, Mhe.Dkt. John Utamwa
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe.Dkt. John Utamwa. |
1(Na. Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya)
……………
Na. Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya
Waziri wa Katiba
na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kwamba Tanzania ina
mgawanyo wa madaraka na unaofuatwa vizuri tofauti na
nchi nyingine.
Akizungumza leo
Novemba 28,mwaka huu wakati alipotembelea Ofisi za Mahakama Kuu Kanda
ya Mbeya, Waziri Mahiga alisema ametembea nchi mbalimbali na kujifunza
kwamba katika nchi yetu mgawanyo wa madaraka (separation of power)
unafuatwa.
‘Mgawanyo wa
madaraka kwa mihimili ya dola, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama
upo na unafuatwa vizuri kulinganisha na nchi nyingine ambapo hata
kuonekana haionekani kabisa na kama ilikuwepo basi ilikufa, alisema
Waziri Mahiga.
Akizungumzia
kuhusu kazi kubwa inayofanywa na Wahe. Majaji ya kusikiliza mashauri
ambapo kuna wakati wanalazimika kufanya kazi hadi kwa zaidi ya saa 18
kwa siku ili kuweza kuwahudumia wananchi na kufikia malengo ya
kitaasisi, alisema anatambua mchango huo na kuwapongeza.
Pamoja na pongezi
hizo, amewataka majaji hao, kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili na utendaji uliotukua kiasi kwamba ikitokea mtu ameulizwa haki
ni nini? katika kutoa majibu amchukue Jaji na kusema hii ndio maana ya
haki.
Hivyo katika
hilo amewashauri Wahe. Majaji kuwa na maadili ya ziada na kuufanya
Mhimili wa Mahakama kutekeleza majukumu kwa viwango vya juu.
Vile vile Waziri
Mahiga amesema kupitia kuongezeka kwa watu na kukua kwa Sayansi na
Teknolojia, nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali
zinazosababisha watu kubuni njia nyingi za uhalifu.
Alisema
changamoto hizo zinasababisha kuwa na uhaba wa majaji kitendo
kinachowalazimu kuwa na makadirio ya kusikiliza mashauri mengi zaidi
tofauti na mipango ya kitaasisi, na kila mmoja kulazimika kufanya
kazi kwa muda mrefu.
Naye Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dkt. John Utamwa, alisema
mikakati ambayo imekuwa ikitumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya katika
kuhakikisha mashauri yanaamuliwa kwa wakati na ubora unaotakiwa ni
uwepo wa miongozo mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa mfano kabla ya
kufika siku 21 nakala za hukumu zinatakiwa kuwa tayari lakini Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya Nakala za Hukumu hutolewa ndani ya siku ambayo hukumu
hutolewa.
Waziri wa Sheria
na Katiba yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, ameambatana na
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Mhe. Biswalo Mganga ambapo wakikagua
Magereza na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafungwa na
Mahabusu.
Katika ziara hiyo, Mhe. Biswalo Mganga amewafutia mashtaka jumla ya watuhumiwa 47.
No comments:
Post a Comment