Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza jinsi ya kuokoa maisha ya mtoto aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya
siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo jijii
Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka kituo cha
Emergency Medical Services Academy kilichopo Mikocheni jijini Dar es
Salaam.
Dkt.
Sylivester Fanya kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy
kilichopo Mkocheni jijini Dar es Salaam akiwafundisha madaktari
na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kuokoa
maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akielezea umuhimu wa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata
tatizo la dharula la kiafya kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI
No comments:
Post a Comment