![]() |
|
Meneja
wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akizungumza
na wageni na waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi wa duka
jipya la kisasa la vyombo vya jikoni
|
Novemba 9, 2019, Dar es Salaam:
Kampuni
ya Kitanzania, Power Systems (T) Ltd, imeshirikiana na wasanifu na
watengenezaji wanaotambulika kimataifa wa vifaa vya jikoni,
Sachsenküchen, kusambaza bidhaa zenye viwango kwenye soko la Tanzania.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa moja ya maduka yake Mikocheni, jijini Dar es
Salaam, Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze
Doring, amesema kwamba ukaribu na wateja utarahisisha kufikisha huduma
zao kwa wateja wa Tanzania.
“Kwa
kuzindua duka la Sachsenküchen, ikiwa ni la kwanza barani Afrika,
tunawaletea Watanzania bidhaa mbalimbali ambazo tunazizalisha. Pia
tunaleta huduma za usanifu wa majiko kutokana na mahitaji ya mteja,”
Doring ameelezea.
Meneja
wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold nae amesema: “Tunafuraha kwa
kuweza kushirikiana na watengenezaji wa vyombo vya jikoni wanaotambulika
duniani ili kuweza kuleta bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwenye
soko. Tanzania pia itafaidika kwa kupata uzoefu na ujuzi watakaoleta
washirika wetu kutoka Ujerumani ambao wana uzoefu wa zaidi ya miaka 100”
Harold
pia ametoa wito kwa Watanzania kutembelea duka hilo jipya la
Sachsenküchen kujionea wenyewe bidhaa bora na kufurahia huduma hiyo
mpya.
“Jikoni
ni mahali ambapo mtu anatakiwa kufanya shughuli zake kwa furaha. Bidhaa
zetu zimetengenezwa kuhakikisha matumizi mazuri ya nafasi huku pia
zikiwa ni za kisasa, zenye kuvutia na kuridhisha wateja,” ameongeza
Harold.
“Hapa
Sachsenküchen kila kitu kinapewa kipaumbele, hususan ubora wa bidhaa
ambazo zinabadilisha na kulifanya liwe ni sehemu halisi ya kuishi,”
amesema.
Sachsenküchen
ni kiwanda kipo Dippoldiswalde, karibu na Dresden, Ujerumani, na
wamekuwa wakisanifu majiko na kutengeneza vifaa vya jikoni kwa zaidi ya
miaka 100.
Tokea
miaka ya 1990, Sachsenküchen imekuwa ikikua huku ikiwa na wafanyakazi
220 na inasavifirisha zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zake nje ya nchi,
mapato ya Euro milioni 40 kwa mwaka huu faida ikiwa ni asilimia 12.









No comments:
Post a Comment