Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (wa mbele) akitoka kuangalia daraja la mto Kanteza
linalowaunganisha wananchi na kituo cha afya cha Laela, Wilayani
Sumbawanga, daraja ambalo limetengewa shilingi milioni 163.2 katika
mwaka wa fedha 2019/2020 huku kazi zikiwa zinaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (wa mbele) akitoka kuangalia daraja la mto Kanteza
linalowaunganisha wananchi na kituo cha afya cha Laela, Wilayani
Sumbawanga, daraja ambalo limetengewa shilingi milioni 163.2 katika
mwaka wa fedha 2019/2020 huku kazi zikiwa zinaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Laela
juu ya adha wanayoipata kabla ya dalaja la mto Kanteza kuanza
kutengenezwa na kutaka kujua maoni yao juu ya ujenzi huo muda mfupi
baada ya kukagua daraja hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo akimkabidhi zawadi ya pesa mmoja wa mtoto wa wananchi aliokuwa
akizungumza nao kupata maoni juu ya ujenzi wa daraja la mto Kanteza
katika mji mdogo wa Laela.
********************************
Wakala wa
Barabara za mijini na Vijijini (TARURA) wametakiwa kuhakikisha Barabara
zote za Vijijini zinapitika mwaka Mzima kwa kufanyiwa matengenezo na
endapo
itashindikana basi ni muhimu kuyapa kipaumbelea maeneo korofi,
hasa katika kipindi hiki cha Mvua jambo ambalo litawasaidia wananchi
kuendelea na shughuli zao za Kiuchumi bila vikwazo.
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha Bodi ya
barabara baada ya wabunge wa mkoa huo pamoja na wenyeviti wa halmashauri
kuilalamikia TARURA juu ya utendaji wake wa kazi pamoja na mipangilio
yao ya bajeti katika kutekeleza majukumu yao.
“Wakala wa
Barabara za Vijijini (TARURA) kuhakiki Barabara zote za vijijini katika
Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa ili kwanza wawe na orodha kamili ya
Barabara za Vijijini na zipo kwenye hali gani,Baada ya kuhakiki wawe na
orodha ya Barabara zilizoingizwa kwenye Mtandao wa Barabara za TARURA
na Barabara zipi hazipo kwenye mtandao wa Barabara za TARURA na
kwanini?,” Alihoji
Aidha alisema
kuwa kwa kufanya hivyo itawasaidia TARURA kuwa na picha ya Barabara zote
za Mkoa wakati wa upangaji wa Bajeti ya mwaka 2020/2021 ili
waweze kuziweka kwenye Bajeti Barabara ambazo zinahitaji Matengenezo.
Wakati
wakiwasilisha malalamiko hayo miongoni mwa wabunge hao walisema kuwa
hawaridhishwi na bajeti inayotengwa na TARURA na hata hiyo inayotengwa
haifikishwi kwa wakati hali ambayo inasababisha hata hicho kidogo
kilichotengwa kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa.
Mbunge wa Nkasi
Kaskazini Mh. Ali Kessy alisema, “Tumepanga bajeti milioni 400 wazilete
zote milioni 400, hauwezi kupanga bajeti milioni 400 unaleta milioni 20,
nimemuuliza mratibu wa (TARURA) Mkoa, mmeleta shilingi ngapi anasema
tumeleta milioni 20 kwenye bajeti ya serikali ya milioni 400, walitenga
kabia daraja la Kavunje, wakadarasai wamekwama daraja haliendelei na
mvua ndio hiyo kama unavyoona.”
Naye Mbunge wa
Nkasi Kusini Mh. Desderius Mipata alisema kuwa wananchi wa kata ya Ninde
watatengwa kutokana na TARURA kushindwa kutenga bajeti kwaajili ya
ukarabati wa barabara inayowaunganisha wananchi wa kata hiyo na kata za
jirani.
“Kwahiyo naomba
mtafute njia yoyote ya dharura ya kuwezesha eneo hilo lipitike hakuna
namna nyingine ya kufanya, nikiwa bungeni daraja la kwenda ninde
lilikuwa limevunjika, nikapiga kelele bahati nzuri walikuja
wakatengeneza kwa pesa kidogo lakini barabara yake haipitiki,”
Alimalizia.
Wakati akitoa
malalamiko yake kwa niaba ya wakandarasi wenzie Bwana Anyosisye Kiluswa
amesema kuwa wakandarasi bado wanazidai halmashauri fedha za matengenezo
ya barabara kadhaa kabla ya barabara hizo hazijahamishiwa kwa TARURA na
kuongeza kuwa halmashauri hizo zilishapewa fedha na serikali lakini
matokeo yake wametumia kwa matumizi mengine.
“Sasa kwa sasa
hivi wakandarasi tunashindwa kutekeleza wajibu wa kufanya kazi kwasababu
pesa zetu wenyewe ni za kuunga unga, ukifanya kazi umelipwa halafu pesa
hiyo hiyo unaichukua unakwenda kufanya kazi sehemu nyingine, sasa
unapokuwa unafanya kazi bila ya kulipwa na nyingine ambazo zipo
wanazitumia kwenye maeneo mengine matokeo yake wakandarasi wa mkoa wa
Rukwa tunaonekana hatufanyi kazi vizuri,” Alisisitiza.
Kwa upande wake
Kaimu mratibu wa TARURA Mkoa wa Rukwa alisema kuwa kwa mwaka wa fedha
2019/2020 jumla ya fedha shilingi bilioni 4.133 kwaajili ya matengenezo
ya barabara km 346.63 na vivuko 48 huku kutoka mfuko wa barabara
zikitengwa shilingi bilioni 1.763 kwaajili ya miradi ya maendeleo ambapo
daraja la mto Kavunja likitengewa shilingi milioni 400 na daraja la mto
Kanteza lilopo Laela likitengewa shilingi milioni 163.2.
No comments:
Post a Comment