Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Bi. Vickness Mayao akifafanua jambo kwa vijana wa kikundi cha
Shilabela wanaonufaika na mradi wa Vijana Maisha ni Kazi unaotekelezwa
na Shirika la Plan International Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi ya
Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipokuwa inatembelea
Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa
utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwezeshaji kutoka Shirika la Amani
Girls Home Bw. Mang’olo Shoma Bahati akieleze jinsi Mradi wa Vijana
Maisha ni Kazi unaotekelezwa na Shirika la Plan International
ulivyowasaidia vijana wa Kikundi cha Shilabela cha Buhongwa wakati Bodi
ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipokuwa inatembelea
Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa
utekelezaji wa miradi katika Mashirika.
Afisa Miradi kutoka Shirika la
Plan International Bw. Nicodemas Gachu akielezea kuhusu utekelezaji wa
Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo wakati Bodi ya Uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipotembelea Miradi inayotekelezwa na
Shirika hilo mkoani Mwanza katika ufuatiliaji wa mwenendo wa utekelezaji
wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye
koti) akikabidhi mchango wa jamii kwa mmoja wa mjumbe wa kikundi cha
Shilabela kilichopo Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi hiyo ilipokuwa
inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia
mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
No comments:
Post a Comment