Mkurugenzi mkuu wa Tasisi ya Elimu
nchini Dr.Aneth Komba akigawa vitabu kwa wanafunzi wa shule ya msingi
Oster bay jijini Dar es Salaam baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na
usambazaji wa vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya
kiingereza kufundishia na kujifunzia
Wanafunzi wa shule ya msingi Oster bay jijini Dar es Salaam wakipitia
kuvisoma vitabu baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na usambazaji wa
vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia
na kujifunzia Mkurugenzi
mkuu wa Tasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akionesha moja ya
kitabu baada ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji na usambazaji wa vitabu
vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia na
kujifunzia.
***************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wamiliki wa shule binafsi,walimu
pamoja wazazi wametakiwa kutumia vitabu vyenye hidhini ya Serikali na
kuachana na tabia ya kutumia vitabu ambavyo havitambuliwi na Serikali.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt.Aneth Komba akizindua kazi ya
kusambaza vitabu vya vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya
kiingereza kufundishia na kujifunzia.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Dkt.Aneth amesema kuwa shule zote zitapewa vitabu bure na vitagawanywa
kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu lakini lengo la
Serikali ni kufikia kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja.
“Tumeandaa vitabu hivihivi kwa
shule za binafsi kwa bei pungufu wakati vitabu ambavyo vitagawiwa kwa
shule za Serikali kwa nyuma vimeandikwa (Not for Sale)”.Amesema
Dkt.Aneth.
Aidha Dkt.Aneth amesema kuwa
Taasisi hiyo inakazi ya kudhibiti ubora wa vitabu hivyo wanakitengo cha
udhibiti ubora ambao kazi yake ni kupitia vitabu na nyaraka zote ambazo
zimeandaliwa kwenda kwenye shule za Tanzania kianzia ngazi ya awali
mpaka vyuo vya Ualimu.
Pamoja na hayo, Dkt.Aneth ametoa wito kwa shule zote ambazo zitapata vitabu hivyo kuvitumia na kuvitunza.
Kwa upande wake Afisa Elimu
Taaluma Mkoa wa Dar es Salaam Bw. George Lukoa amewasihi wadau wa Elimu
hasa Wanafunzi wasome kwa bidii ili kuweza kuendana na mfumo wa Elimu
bure unaotolewa na Serikali kwani Serikali imekuwa ikitumia gharama
kubwa kuwezesha Elimu bure kwa wanafunzi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment