Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za
lugha ya Kiswahili na taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio
lililofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
akizindua Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili
katika hafla iliyofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini
Kenya. Kuanzia kushoto ni Kiongozi wa Walio wengi Bungeni (Majority
Leader), Mhe. Aden Duale, Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na
Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
akizungumza na Waheshimiwa Wabunge na Wageni waalikwa (hawapo kwenye
picha) katika hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za
lugha ya Kiswahili na taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio
lililofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(katikati) akiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya za lugha ya Kiswahili na
taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati tukio lililofanyika leo
katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya. Kulia ni Spika wa Bunge la
Kenya, Mhe. Justin Muturi na Kushoto ni Kiongozi wa Walio wengi Bungeni
(Majority Leader), Mhe. Aden Duale.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
akizindua taarifa za Mwaka za Utendaji Kazi wa Kamati katika hafla
iliyofanyika leo katika Bunge la Kenya, Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni
Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi na Naibu Spika wa Bunge la
Kenya, Mhe. Moses Cheboi.
No comments:
Post a Comment