Pages

Tuesday, October 1, 2019

SERIKALI YATENGA BILIONI 65 ZA KUJENGA MINARA YA MAWASILIANO



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyetangulia mbele) akitoka kukagua mnara (unaoonekana pichani nyuma) wa kijiji cha Mlaga, kata ya Nyampande wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, Sengerema mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa ofisini kwake akifurahi baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) kitabu chenye orodha ya minara iliyojengwa na UCSAF. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella
Wananchi wa Nyampande wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) akiwahamasisha kusajili laini za simu zao kwa alama za vidole wakati wa ziara yake Sengerema, Mwanza
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akihamisha wananchi wa Nyampande kusajili laini za simu zao kwa alama za vidole wakati wa ziara yake Sengerema, mkoani Mwanza
…………………………..
Na Prisca Ulomi, Mwanza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi bilioni 65 kwa ajili ya kujenga minara ya mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini ili kuongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kukuza uchumi na kufanikisha utoaji wa huduma za
Serikali kwa wananchi, wananchi waweze kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe, kuwasiliana na Serikali yao na kurahisisha uendeshaji wa shughui za kijamii
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akikagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye kata ya Nyampande iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza. 
Mwenyekiti wa kijiji cha Malaga kilichopo kwenye kata ya Nyampande, Mathayo Thobias ameishukuru Serikali kwa huduma ya mawasiliano wanayoipata kwa kuwa wameingia kwenye mawasiliano bila kusua kusua baada ya kusimikwa kwa mnara wa mawasiliano kwenye kata hiyo na amekiri kuwa mnara wanafurahia uwepo wa mnara huo kwa kuwa mbali na kuwapatia huduma za mawasiliano pia umekuwa chanzo cha mapato ya kijiji ambapo Serikali ya kijiji inapata shilingi milioni 3.6 ambazo inalipwa na kampuni ya Vodacom inayomiliki mnara huo
Nditiye amesema kuwa, tayari Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 65 za kujenga minara ya mawasiliano ipatayo 1,222 kwenye kata 521 sehemu mbali mbali nchini nzima kwa kuupa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ruzuku ya kuzipa kampuni za simu za mkononi fedha hizo kupitia utaribu uliowekwa, kwa kuzingatia vigezo na masharti ya zabuni ambapo UCSAF ilitangaza zabuni ya kujenga minara hiyo na kampuni za simu ziliomba zabuni hizo ili kujenga minara hiyo nah ii karibuni watapatiwa fedha hizo ili kuanza ujenzi wa minara
Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alipofika kumsalimu, Nditiye alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakiisha kuwa Sekta ya Mawasiliano inaongeza mchango wake kwenye pato la taifa kwa kuongeza kiwango cha uchangiaji kutoka asilimia 13.1 kwa mwaka 2017/2018 kwa kushika nafasi ya tatu
“Hapa tulipo wote tuna simu za mkononi na hakuna atakayekaa zaidi ya nusu saa bila kushika simu yake ya mkononi,” amesema Nditiye. Amefafanua kuwa lengo la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ya mfano na tayari nchi nyingi za Afrika zinajifunza kwetu kwa Sekta ya Mawasiliano na dhamira ya Serikali ni kuendeleza Sekta hii ili kwenda sambamba na nchi zilizoendelea duniani ambapo hadi sasa Tanzania iko vizuri kati ya nchi chache za Afrika kama vile Afrika Kusini na Mauritius kwa upande wa mawasiliano
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemweleza Nditiye kuwa mkoani kwake usikivu wa mawasiliano uko vizuri, mawasiliano yanasikika kwa kiwango cha juu sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma
“Zamani hata likitokea tukio inachukua wiki kufahamu ila sasa ni saa chache tu tunapata taarifa na kushughulikia,” amesema Mongella. Nikiri wazi kuwa mawasiliano yamesogeza wananchi karibu na Serikali yao
 Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemweleza Nditiye kuwa Sekta ya Mawasiliano ni Sekta wezeshi, sisi Sekta yetu ya viwanda na biashara inategemea sekta yako ya mawasiliano na inatuwezesha kuingia na kutumia fursa ya soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, hivyo kuongeza soko la ajira na kukuza uchumi wa taifa letu na kwa vile Mwanza ni mkoa wa kimkakati ni dhahiri kuwa mawasiliano yanaongeza chachu ya biashara
Naye Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi wilayani Sengerema, Ashura Kajuna alimueleza Nditiye maara alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa kumekuwa na shida ya upatikanaji wa vocha za mtandao wa TTCL hivyo amemuomba Nditiye kuhakikisha kuwa vocha hizo zinapatikana kwa kuwa huduma za za sauti na data TTCL ni za gharama nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine
Nditiye amesema kuwa ni jukumu la taasisi za Serikali kupeleka mahitaji kwa wananchi kuendana na matakwa yao, hivyo ameliagiza Shirika la TTCL kuhakikisha kuwa kila palipo na laini za simu za TTCL kuwe na vocha. 
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema, Allan Augustino, amemuomba Nditiye kuhakikisha kuwa maeneo ya pembezoni yanapata huduma za data ili kuweza kufanikisha huduma za intaneti adala ya kupata huduma za sauti tu
Nditiye anaendelea na ziara yake mkoani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wanachi wasajili laini za simu zao na kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi

No comments:

Post a Comment