Pages

Wednesday, October 2, 2019

SERIKALI YATAJA MAENEO YANAYOASHIRIA KUVUMBULIWA RASILIMALI YA MAFUTA NCHINI TANZANIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.  Kongamano hilo linawakutanisha wadau zaidi ya 592 kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo Austaralia, Brazili, Canada, China, Visiwa Vya Comoro, Ghana. Mengine ni Itali, India, Japani, Kenya, Msumbiji, Netherand, Nigeria, Afrika Kusini, Oman, Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Nishati na Madini Meldard Kalemani akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea. Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2. Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora. Dk Kalemali ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi. “Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani. Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi. "Tunawakaribisha wawekezaji zaidi wajitokeze katika sekta hii ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na kuzidi kutoa ajira wa jamii," amesema. Meza kuu: Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim, Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na Bi. Irene Batete aliyemwakilisha waziri wa Nishati Nchini Uganda.  Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Bi. Irene Batete aliyemwakilisha Waziri wa Nishati Nchini Uganda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim ambao ndiyo waandaaji akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. 
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.

No comments:

Post a Comment