Eric Msuya – MAELEZO
Naibu waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Stellah Manyanya amewataka wadau wa Sekta hiyo kutumia
mfumo mpya wa kukusanya Taarirfa za Kibiashara Nchini kwa lengo la
kupiga hatua kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati.
Kuanzishwa kwa mfumo huo ujulikanao kama Trade Information Module,
ni utekelezaji wa
makubaliano ya kimataifa yaliyopo kwenye mkataba wa
uwezashaji wa Kibiashara unaosimamiwa na Shirika la Biashara Duniani.
Manyanya aliyasema hayo jana,
Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Wafanyabaishara na Wadau
waBiashara, kuhusu mfumo wa utoaji wa Taarifa za Kibiashara Nchini,
ambapo alisema, mfumo huo mpya utasaidia utunzanzaji na upatikanaji wa
taarifa za Leseni pamoja na Vibali mbalimbali vya kufanyia
BiasharaNchini.
“kama manavyojua, upatikanaji wa
Taarifa ni muhimu sana katika kufanya maaamuzi ya kila jambo hivyo
uwepo wa Taarifa hizi za Biashara mahali pamoja utasaidia
Wafanyabiashara kujua mahitaji, utaratibu na mahali pakupata vibali
mbalimbali” alisema Mhe. Stellah
Alisema mfumo huu utaliwezesha
Taifa kupata Fedha za kigeni sambamba na kumsaidia mfanyabiashara kujua
taratibu na masharti ya kuingiza Bidhaa zao Nchini kupitia Masoko ya Nje
ya Nchi.
Sambamba na hilo, Mhe. Stellah
aliwataka Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali kutumia mfumo huo vizuri
kwani utaleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Biashara Nchinipamoja na
kuondoa kero mbalimbali.
“lakini pia mfumo huu utaongeza
ukaribu baina ya Wafanyabaishara na Ofisi za Umma, utaongeza ufanisi na
kupunguza gharama za Kibiashara, utapunguza muda anaotumia
Mfanyabiashara kupata Leseni, hivyo kwa ujumla mfumo huu utaboresha
Mazingira ya Kibiashara Nchini kwa kuchangia Uchumi wa Nchi” alisema Mhe
Stellah.
Pamoja na hilo, Serikali ya awamu
ya Tano, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, inaendelea kufanya
jitihada mbalimbaliza za kuboresha Mazingira ya Kibiashara Nchini
(Blueprint For Regulatory Reform to Improve Business Environment) ili
kuweza kuwavutia wawekezaji wa ndani na Nje ya Nchi kuja kuwekeza hapa
kiurahisi.
“tunafanya jitihada nyingi sana ili kuboresha mazingira nchini hususan mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania” alisema Manyanya.
No comments:
Post a Comment