Pages

Tuesday, October 29, 2019

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKUTANA NA KAMATI KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA



Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (wa tatu kutoka kulia) wakimsikiliza Adam Mbyallu wa  Sahara Ventures  walipotembelea Hubs za Sahara Ventures, DTBI,Jenga Hub na Seedspace zote za jijini Dar es  Salaam, Ziara hiyo iliandaliwa na mfuko wa ubunifu (HDIF) unaojishughulisha na kukuza ubunifu na kusaidia wabunifu nchini (Innovation ecosystem).
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akichangia mada wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofanya ziara ya kujifunza   katika  ofisi mbalimbali za uvumbuzi (innovation hubs) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Adam Mbyallu wa Sahara Ventures. Ziara hiyo iliandaliwa na program ya HDIF inayojishughulisha na kusaidia wavumbuzi wa teknolojia nchini.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc  wakimsikiliza  Iddy John wa atamizi ya DTBI wakati akifafanua juu ya uvumbuzi wa Teknolojia unaoweza kuwaunganisha  wafanyabiashara kwa pamoja  wakati wafanyakazi wa vodacom walipofanya ziara ya kujifunza katika  Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga  na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliandaliwa na program ya HDIF inayojishughulisha na kusaidia wavumbuzi wa teknolojia nchini.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi  (wa pili kushoto)  wakimsikiliza  Andrew Tesha wa atamizi ya  DTBI wakati akifafanua juu ya uvumbuzi wa Teknolojia inayoweza kuwaunganisha wafanyabiashara kwa pamoja  wakati wafanyakazi wa vodacom walipofanya ziara ya kujifunza katika  Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga  na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliandaliwa na program ya HDIF inayojishughulisha na kusaidia wavumbuzi wa teknolojia nchini.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC,  wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rossalyn Mworia  (kulia aliye kaa) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Jenga Hub, Nancy Sumari  (kushoto) wakati alipokuwa akifafanua jinsi walivyofanya  uvumbuzi wa  kuwafundisha watoto wa shule kwa kutumia Teknolojia (Innovation ) wakati wafanyakazi hao walipofanya ziara ya kujifunza  katika  Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga  na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliandaliwa na program ya HDIF inayojishughulisha na kusaidia wavumbuzi wa teknolojia nchini.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC,  wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rossalyn Mworia  ( wa kwanza kulia aliyekaa) wakimsikiliza meneja wa Hub ya Jenga Lupyana Mbembati wakati alipokuwa akielezea namna  wanavyotumia   Teknolojia kuwafundisha watoto wa shule wakati wafanyakazi hao walipofanya ziara ya kujifunza  katika  Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga  na Seedspace zote za jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliandaliwa na program ya HDIF inayojishughulisha na kusaidia wavumbuzi wa teknolojia nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa katika ofisi za hub ya Seedspace  wakati walipofanya ziara ya kujifunza maswala ya Teknolojia kwenye Hubs za Sahara Venture, DTBI, Jenga  na Seedspace zote za jijini Dar es  Salaam.

No comments:

Post a Comment