************************
Na Queen Lema Arusha
Aliyekuwa waziri wa
mipango wa serikai ya mpito ya Rwanda Bw. Augustine Ngirabatware
ameshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wenye uwezo wa kuaminika
katika kikao cha
rufaa cha mahakama ya kimataifa inayoshughulikia
masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari ili kuweza kubatilisha hukumu
ya awali anayendelea kuitumikia.
Rais wa mahakama hiyo
Jaji Theodor Meron amesema kuwa kupitia kifungu cha sheria namba 147
ya mwenendo wa ushuhuda Ngirabatware ambaye aliita mashahidi sita
wameshindwa kutoa ushahidi wa ukweli unaounga mkono hoja mpya ya
kubatilisha ushahidi wa awali uliotolewa kuwa sio wa kweli na hivyo
hukumu ya awali bado inaendelea.
Mnamo Desemba 2012
mahakama ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR)ilimtia hatiani
Ngirabatware kwa kosa alilolifanya mwaka 1994 la kufanya uchochezi wa
moja kwa moja wa kufanya mauaji ya kimbari na makosa ya ubakaji na
kuhukumiwa miaka 35 jela na baadae Desemba 2014 mahakama ya kesi za
masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari iliondoa kosa la ubakaji na
kubaki na kifungo cha miaka 30.
Aidha Julai 8 mwaka
2016 Ngirabatware aliwasilisha ombi la kupitia upya hatia yake na Juni
mwaka 2017 mahakama hiyo iliridhia kusikiliza kusikiliza shauri lake
upya ambapo kesi hiyo ilianza kusikilizwa september 16 hadi 27 mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment