Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Katibu
Mkuu OR-TAMISEMI (Afya), akifungua kikao cha Wataalam Wafamasia katika
ukumbi wa Mikutano wa OR-TAMISEMI (Picha zote na Atley Kuni-TAMISEMI).
Mkurugenzi wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Ntuli Kapologwe, akitoa maneno ya
utangulizi juu ya kikao hicho kabla yakumkaribisha Naibu Katibu Mkuu
kufungua kikaokazi hicho.
Wafamasia wa Mikoa wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu hayupo pichani wakati wa kikao cha wataalam hao mjini Dodoma.
****************************************
Na Atley Kuni- TAMISEMI.
Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy
Gwajima, amewataka Wafamasia wa Mikoa kote nchini kupambana na kukomesha
watu
wanaofanya ubadhilifu wa dawa zinazotolewa na serikali kwenda
kwenye sehemu za kutolea huduma za afya sambamba na kutafsiri falsafa ya
hapa kazi tu kwa vitendo.
Akizungumza
katika kikao kazi cha wataalam hao kinachofanyika mjini Dodoma, alisema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ametekeleza vema ilani ya Chama cha Mapinduzi kwakuijali na kuipa
kipaumbele sekta ya afya na ndio maana katika mwaka wa fedha 2019/20
serikali imepitisha bajeti ya Shilingi bilioni 57.4 ambapo katika
mgawanyo eneo la dawa ni miongoni mwa vipaumbele vitatu vilivyo pewa
umuhimu.
“Sasa tusimhujumu
Mhe. Rais ambaye ameshafanya kazi kubwa na sisi tuliomo ndani ambao
tumewekwa kusimamia tunaujuzi na utaalam sehemu ambayo yeye hawezi
kuingia, watu wanaiba dawa tunawaangalia, wanaiba vitendanishi
tunawaangalia, tutakuwa hatutimizi wajibu wetu kama matazamia yake naya
wanachi yanavyotaka” alisema Gwajima.
Gwajima amewataka
Wafamasia hao kutumia mfumo wa Ugavi wa dawa wa (elmis) ambao kimsingi
taarifa zote za dawa zinaingizwa na kutumika kama muhtadha wa kuombea
dawa kwa kila robo. Alisema mfamasia wa Mkoa atakuwa na wajibu wa
kuhalalisha maombi ya dawa kwenda MSD kila mara, huku akiitaja mikoa ya
kuanzia katika zoezi hilo ni pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Kagera
na Geita.
“Tunataka kufanyika kwa Medicine Audit kila
robo na taarifa yake kwa kila mkoa iwasilishwe OR-TAMISEMI” alisema
Gwajima na kuongeza kuwa “lengo ni kuchakata taarifa za mifumo ya dawa
ili kubaini kama kuna hazina ya dawa za kutosha au lah, ili kuweza
kusaidia maeneo ambayo yanaupungufu wa dawa.” Alisisitiza Gwajima.
Katika hatua
nyingine Gwajima alisema Serikali hivi sasa ipo katika maboresho makubwa
ya mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Afya (Government of Tanzania Health Management Information System-GoTHOMIS) ambao baada ya kukamilika kwake mfumo utatoa taarifa nyingi za makusanyo ya fedha za dawa mpaka ngazi ya mtumiaji wa mwisho.
Awali kabla
yakumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya na Ustawi wa
Jamii OR-TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe, alisema Sekta ya Afya imekuwa
miongoni mwa sekta zilizo pewa kipaumbele na Mhe. Rais hivyo kama
wataalam lazima tuoneshe kwa vitendo kuwa Mhe. Rais hajakosea katika
hili.
“Mtakumbuka ziara
ya mwanzo kabisa Mhe. Rais, alijielekeza katika sekata hii muhimu kwa
mustakabali wa maendeleo nchi hasa wakati huu tunapoelekea katika uchumi
wa kati ifikapo 2025. Lakini hakuishia hapo toka ameingia madarakani
imeendelea kutenga fedha kwaajili ya kujenga na kukarabati vituo vya
kutolea huduma za afya, ambapo katika mwaka wa fedha 2017/18 vituo vya
afya 352 zikiwepo Hospitali 9, Vituo vya Afya 304 na Zahanati 39
zilikarabatiwa, lakini hivi sasa vituo vinavyo jengwa na kukarabatiwa
vimefikia 470 zikiwemo hospitali 67 mpya za Halmashauri ambazo zitakuwa
na idara kamili ya dawa” alisema Kapologwe.
Kikao cha
Wafamasia kimetayarishwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ushirikiano na
wadau wa maendeleo, lengo likiwa nikuweka mipango ya kuhakikisha mianya
ya ubadhilifu wa dawa inakomeshwa lakini pia kuweka mikakati endelevu ya
upatikanaji wa dawa katika sehemu zote za kutolea huduma za afya.
No comments:
Post a Comment