Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiwa amesimama mbele ya
nyumba zilizojengwa wilayani Namtumbo ikiwa ni Utekelezaji wa
agizo la
Rais Dkt. John Magufuli la kutaka kujengwa nyumba za askari wa vyeo vya
chini nchi nzima ambapo alitoa kiasi cha fedha Bilioni 10 ili ziweze
kutumika katika ujenzi huo. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma, Kamishna Msaidizi, Simon Marwa na wengine ni viongozi wa jeshi
hilo mkoani Ruvuma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
***********************************
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
Shilingi Bilioni
10 zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Askari wa Vyeo vya chini zimeanza
kutumika mkoani Ruvuma huku jumla ya nyumba sita zikiwa zimejengwa
katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Rais Magufuli
aliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha wakati akizindua Kituo cha Polisi
cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha mwezi April mwaka huu.
Akizungumza leo
wakati wa ziara ya ukaguzi wa nyumba hizo mkoani Ruvuma, Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alisema tayari nyumba
hizo zimekamilika na tayari ujenzi unaendelea mikoa yote nchini ambako
ilibainika kuna changamoto ya makazi ya askari
“Rais wetu
aligundua changamoto ya askari wetu hawa hasa wa vyeo vya chini,akatoa
kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa jeshi la polisi,leo nimefika hapa
kuangalia matumizi ya fedha hizo na nimeridhishwa na hatua ya ujenzi
ulikofikia kwani nyumba zimekamilika na tayari nimeona baadhi askari
wetu washahamia,”alisema Masauni
“….tunatembea
nchi nzima kuona nyumba hizo zimefikia hatua gani lengo ni kuona askari
wetu wanahama katika makazi duni na kuhamia nyumba hizi mpya ambazo
serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa hiyo changamoto.”
Aliongeza Masauni
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Kamishna Msaidizi
Simon Marwa alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa
kiasi hicho cha fedha ambapo wao walipata mgao wa Shilingi Milioni
150/= huku akitaja idadi ya nyumba walizojenga.
“Nyumba
zishakamilika na askari wa vyeo vya chini wameshahamia kama maelekezo ya
Mheshimiwa Rais yalivyosema, hapa kuna nyumba sita ambazo kuna vyumba
viwili vya kulala, sebule na chumba cha kulala kwa kila nyumba,” alisema
RPC Simon
Kamanda Simon
alisema mkoa wa Ruvuma una wilaya tano za Songea, Tunduru, Mbinga,
Namtumbo na Nyasa huku mapendekezo ya nyumba hizo kwa mkoa huo
zikijengwa wilayani Namtumbo ambako changamoto ya makazi ilikua kubwa
tofauti na wilaya zilizobakia.
No comments:
Post a Comment