Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akifungua kongamano la wazee
lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara katika
mfulululizo wa maadhimisho ya Kimataifa ya Wazee.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini
kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. naftari
Ngondi akifafanua jambo wakati wa kongamano la wazee lililofanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara.
Baadhi ya washiriki kongamano la wazee linaloendelea katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mtwara.
Mzee Seifu Nantapika Katibu
Mtandao wa Wazee Mkoa wa Mtwara akitoa salamu kwa wazee washiriki
kongamano la wazee lililofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani
Mtwara.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………
Na Mwandishi Wetu Mtwara
Baraza la Wazee limeiomba Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kuwasaidia wazee kwa kuwapatia ...
pensheni jamii
itakayowasaidia katika mahitaji yao ya kila siku kwa wazee ambao
hawakuwa katika ajira rasmi.
Hayo yamebainika leo mkoani Mtwara
wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wazee kuelekea maadhimisho ya Siku
ya Wazee Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Benki ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya
Kongamano hilo Katibu wa Baraza la Wazee la Halmashauri ya Mji wa Kahama
Mzee Anderson Lyimo amesema kuwa wazee wamelitumikia taifa katika
Nyanja mbalimbali hivyo ni suala la muhimu kwa Serikali kutafakari na
kuwapatia wazee pensheni jamii itakayowasaidia kutatua changamoto
ndogondogo za kimaisha.
Mzee Lyimo ameongeza kuwa pensheni
ya jamii kwa wazee itawasaidia wazee kuondokana na utegemezi kwa jamii
hasa kuondokana na wimbi la wazee ombaomba ambalo kwa kiasi kikubwa
hutokana na wazee kukosa fedha za kujikimu kwa mahitaji yao madogo
madogo.
“Tunakuomba Mhe. Rais Magufuli
tukumbuke katika suala la pensheni jamii kwetu sisi wazee itatusaidia
sana kwa mfano wenzetu wa Zanzibar wanapata elfu 20 angalau kupata
kuliko kukosa kabisa” alisisitiza Mzee Lyimo.
Mzee Lyimo amesisitiza kuwa jamii
inawajibu wa kuwalea na kuwatunza wazee kwa asilimia kubwa na kuwaasa
vijana kutowatelekeza wazazi wao wakati wanapozeeka na wajue kuwa ni
wajibu wao kuwalea na kuwatunza wazee kama wao walivyotunzwa wakiwa
watoto.
Akifungua Kongamano hilo Katibu
Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa
Kongamano hilo litumike kutafakari kwa jinsi gani taifa litafanya
kuwalea na kuwatunza wazee na kupata njia sahihi za kupambana na
changamoto zinazowakabili.
Dkt. Jingu ameongeza kuwa ni
muhimu sana kwa taifa kujadili suala la kuwaenzi na kuwatunza wazee
pamoja na kuhakikisha wanakuwa na ustawi mzuri katika maisha yao ili
waendelea kutoa mchango wao katika ujenzi wa taifa.
“Naomba tujadilia pia wajibu wa
jamii katika kuwatunza na kuwaenzi wazee kama wazazi wao ndugu na jamaa
waliochangia nguvu zao katika ujenzi wa taifa letu” alisema Dkt. Jingu
Dkt. Jingu ametaja jitihada hizo
kuwa ni pamoja na Sera ya matibabu bure kwa wazee, uwepo wa mabaraza ya
wazee na mapitio ya Sera ya wazee ili kuhakikisha kuwa inajitosheleza
lakini pia Serikali ina makao 17 ya wazee ambayo yanapokea wazee
wasiokuwa na ndugu wala jamii ya kuwahudumia.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Chama cha Wazee na Wastaafu mkoa wa Arusha Bi. Miriam Urio amewataka
vijana nchini kuachana na vitendo vya imani za kishirikiana kusababisha
vifo kwa wazazi wao kwasababu ya uzee bali wawatunze na kuwalea wazee
wao kama wao walivyowatunza wakiwa watoto.
No comments:
Post a Comment