Maofisa wa Benki ya NMB wakifurahi
pamoja na Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar,
Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani
kwa udhamini wao.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Dar es Salaam, Badru Idd (mwenye miwani) akisalimiana na Makamu wa Pili
wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi rasmi wa
Maonesho ya pili ya ‘Zanzibar Tourism Show’ Visiwania Zanzibar.
………………….
UONGOZI wa Benki ya NMB umesema
kuwa unazidi kuboresha mifumo ya huduma zao za
kadi ili kuhamasisha
watalii pamoja wananchi wa kawaida kutumia kadi kwenye malipo na
ununuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
Idara ya Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir wakati
akizungumza kwenye maonesho ya Utalii visiwani Zanzibar, ambapo benki
hiyo ni moja wapo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyofika tamati
siku ya Jumamosi.
Alisema kutokana na ukuaji wa
Teknologia Duniani, ndivyo wanavyo buni mbinu zitakazo wawezesha wateja
wao kupata huduma bora na za kimataifa. Vilevile, mifumo ya Kidigitali
na matumizi ya kadi za MasterCard ambazo zinatumika kitaifa na
kimataifa zimekua zikiondoa usumbufu kwani huduma hizo zinaweza
kutumikaa ndani na nje ya nchi.
Benki ya NMB benki hivi sasa ipo
karibu na wananchi mjini na vijijiNI hivyo kuingia katika masauala ya
utalii, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuzidi kujitangaza na kuvutia wateja
wengi zaidi pamoja na wageni wanaofika nchini.
Naye Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar- Balozi Seif Ali Iddi ameomba mashirikiano na taasisi nyingine
katika kutangaza utalii wa Zanzibar ili kuongeza idadi kubwa ya watalii
Zanzibar.
Alisema wananchi wa Zanzibar
wananufaika na utalii kupitia sera ya Utalii kwa wote na kubainisha kuwa
sera hiyo ipo wazi kuweza kunufanisha wananchi hasa kwa kuwa na
usalama wa nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari,
Utalii na Mambo ya Kale- Mahamoud Thabiti Kombo alisema kuwa maonyesho
hayo ni agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ambapo lengo ni
kuitanganza Zanzibar kiutalii baada ya mafanikio makubwa ya waka jana.
Alisema kuwa maonesho ya kila
mwaka yanawasadia wajasiriamali wadogo wadogo kujitangza kupitia utalii
ili waweze kunufanika na matunda ya utalii kwa kuuza bidhaa na kukuza
biashara zao.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi
la Zanzibar – Abdalla Duchi, amewataka wananchi wa
Zanzibar kuchangamkia fursa za utalii zinazopatika nchini ili
kujikwamua na umaskini .
Amewataka wajasiriamali wadogo
wadogo na wa kati kutumia fursa zinazotolewa na Benki hiyo katika
maeneo mbalimbali kwa kujisajili kuwa mawakala, ambapo itafungua fursa
za ajira sambamba na kutoa huduma kwa wananchi wa kawaida ikiwemo
watalii wanaokuja kutembea Zanzibar.
Aliongeza kuwa benki ya NMB ina
wateja zaidi ya milioni tatu huku ikiongoza kwa matawi mengi – 229
nchini, yakiwemo NMB Zanzibar, NMB Mwanakwerekwe na NMB Chakechake-
Pemba, huku ikiwa na jumla ya mawakala 84 Zanzibar kwa jumla ya idadi ya
mawakala 6000 nchi nzima.
#NMB Karibu Yako
No comments:
Post a Comment