Pages

Sunday, September 29, 2019

SELLA MJASIRIAMALI ALIYEINUKA KIUCHUMI KUPITIA SIDO,AANZA NA MTAJI WA LAKI TANO


Na.Alex Sonna,Dodoma
NI UTHUBUTU ndio umepelekea kupiga hatua moja kwenda nyingine, hayo ni maneno ya Mjasiriamali Sella Mkisi ambaye ni Mkurugenzi wa Unique & Superior Bakery jijini hapa inayojihusisha kutengeneza vitafunwa na kusambaza katika maeneo ya ndani na nje ya jiji la Dodoma
Ni kama hadithi lakini ni ukweli usiopingika kutokana na Mjasiriamali Sella Mkisi ambaye anasema mafanikio yake yametokana na juhudi za Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO)
ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kumtoa hatua moja kwenda nyingine, katika suala zima la ukuaji kiuchumi katika ujasiriamali anaofanya.
Alifanyaje mpaka kufikia hapo ni baada ya kupeleka wazo lake la kutaka kujifunza kutengeneza mikate maandazi pamoja vitu mbalimbali akitumia fursa ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambayo mkoa umeyaainisha na kutoa fursa kama mjasiriamali unaona unaweza kumudu na kuingia kwenye ushindani wa soko la kimataifa kadri siku zinavyokwenda kujitokeza kuwekeza.
Wazo lake la kutengeneza vitafunwa kama mikate,maandazi na keki lilionekana kuwa lulu baada ya kuongeza ujuzi SIDO,na baada ya kuhitimu mafunzo yake alianza kuchukua mkopo wa laki tano toka SIDO kama mtaji wake wa kutengeneza mikate,maandazi na baadae keki ambazo anaziuza sehemu mbalimbali hapa jijini na nje ya jiji la Dodoma.
Ni kama mzaha alianza lakini kadri siku zinavyokwenda anazidi kutanua wigo wa ujasiriamali anayofanya.
Katika mahojiano na Mkurugenzi wa Unique & Superiol Bakery Sella Mkisi anasema hakuna kitu kikubwa kama uthubutu,ukijaribu kitu unachotaka kufanya basi ni lazima kitafanikiwa kwa sababu tayari umeweka nia ya kusudio lako ambalo unahitaji kufanya katika ujasiriamali.
Anasema ukifanya hivyo ni dhahiri kwamba unahitaji kupata mafanikio katika biashara yoyote unayotaka kufanya isipokuwa uzingatie nini unahitaji kuwekeza.
Akisimulia Sella anasema yeye alianza na mtaji wa laki tano tu lakini ndoto yake ni kuwa Mjasiriamali mkubwa katika biashara ya mikate na maandazi anayofanya hivi sasa hapa jijini pamoja na kusambaza nje ya jiji la Dodoma na inaonekana kupendwa na watu wengi kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
“Nivigumu kuamini hiki ninachosema lakini ni ukweli nashauri vijana wenzangu kuwa na uthubutu wa kile wanachofikiria kufanya wafanye wasisite,” amesema Sella.
Anasema hivi sasa taifa linaelekea katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo ni vema vijana wengi kuweka uthubutu katika ujasiriamali wanaofikiria kufanya ili kutumia fursa ambazo zinatangazwa na jiji la Dodoma ili kuweza kusonga mbele katika kile wanachofikiria kufanya badala ya kusubiri ajira toka serikalini au kampuni yoyote binafsi.
Anasema kinachotakiwa ni kufikiria jinsi gani ya kufanya katika ujasiriamali unaohitaji kufanya ikiwemo kutumia fursa za mikopo ambazo zinatolewa na taasisi mbalimbali hapa nchini ili kufikia lengo unalohitaji kufanya

No comments:

Post a Comment