Pages

Sunday, September 29, 2019

Mafunzo ya kukuza Biashara ya TBL Yazidi Kunufaisha Wajasiriamali Wengi Nchini



Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika mashariki Bi.Edith Bebwa,akiongea wakatiwa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyowalenga zaidi wamiliki wa mabaa na Mameneja wao wakipokea vyeti vya ushiriki
Wahitimu katika picha ya pamoja wakati wa mahafali hayo
………………
Kampuni ya Bia Tanzania chini ya kampuni  ya kimataifa ya ABInBEV, Mwishoni mwa wiki iliwatunuku vyetiwahitimu waMafunzo ya kukuza Biashara kwa wajasiriamali wadogo
yaliyoendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaan na Dodoma.
Haya ni mahafali ya pili tangu kuanzishwa kwa programu hii ya kukuza biashara kwa wajasiriamali wadodo hapa Tanzania mwaka Jana, 2018.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika Mashariki Bi.Edith Bebwa alisema, “Programu hii ambayo inajulikana zaidi kama RDP, imefanikiwa kuwafikia washiriki 183 ikiwa ni ongezeko la 11% ukulinganisha na mwaka jana. Wengi wa washiriki ni wamiliki na wasimamizi wa baa mbalimbali kutoka katika mikoa hii miwili ya Dar es salaam na Dodoma.
“Leo tarehe 26 Septemba 2019, tunayo furaha kuwatunuku vyeti wajasiriamali hawa wa Dar es salaam waliopata mafunzo  kwenye wilayani zao yaani  Temeke (iliyojumuisha Temeke na Kigamboni),Kinondoni,Ubungo na Ilala.Washiriki hawa wamepatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na kufundishwa kitalaam ili yaweze kusaidia kuendelezana kukuza biashara zao na hatimaye kuchangia zaidi uchumi wa taifa kupitia kodi na ajira. Mafunzo haya yalitolewa katika namna mbili, moja mafunzo ya nadharia darasani na pili mafunzo na ushauri katika maeneo yao ya biashara”. Alisema Bebwa.
Kwa upande wake kiongozi wa TAPBDS taasisi iliyosimamia uendeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Joseph Migunda alisema, “Mafunzo haya yana maudhui yaliyoendana na utendaji na mahitaji katika aina hizi za biashara. Mzunguko wake umechukua takribani miezi minne kuanzia mwezi wa Sita hadi wa Tisa. “Tunaimani kwamba wengi wa washiriki watanufaika nayo na tayari tunashuhuda mbalimbali kwa baadhi yao ambao wamechukua hatua tofauti na kufanyia kazi elimu na ushauri waliopata kwa ajili ya maboresho. Tunashukuru ubunifu huu wa TBL na uamuzi wao wa kutumia wataalamu wetu katika kuwezesha haya yote.” Alisema

No comments:

Post a Comment