Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi wakati akifungua rasmi uzinduzi
wa programu ya Huduma za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information
and Services for Africa (WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania.
Mratibu wa programu ya WISER kwa Nchi za Afrika Mashariki, Ndugu. John Mungai akizungumza wakati wa uzinduzi
wa programu ya Huduma za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information
and Services for Africa (WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania.
Rais wa TMS Dkt. Burhani Nyenzi akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya Huduma za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information and Services for Africa (WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania. |
Wadau mbalimbali wakizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya Huduma za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information and Services for Africa (WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania. |
*******************
Tarehe 29/08/2019 Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Hali ya
Hewa Tanzania (TMS) kupitia programu ya “Weather and Climate
Information Services” (WISER), imejipanga katika kuongeza nguvu ya
utoaji hudumza za
hali ya hewa ili kufikia wananchi wengi zaidi.
Hayo yalizungumzwa na mkurugenzi
mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
Dkt. Agnes Kijazi wakati akifungua rasmi uzinduzi wa programu ya Huduma
za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information and Services for Africa
(WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza,
Dar es Salaam, Tanzania.
‘Programu hiyo itaiwezesha Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania kusambaza taarifa za hali ya hewa pamoja na
kuelimisha wadau mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya
hewa hususan katika sekta za Kilimo, Usafiri majini, Udhibiti wa
majanga, Maji na Nishati hivyo itaongeza nguvu katika kuwafikia wananchi
wengi’,alizungumza Dkt. Kijazi.
Aidha, aliendelea kueleza kuwa
madhumuni makubwa ya program ya WISER Kitaifa ni kuhakikisha kunakuwa na
matumizi sahihi ya tarifa za hali ya hewa katika sekta mbali mbali za
maendeleo kwa lengo la kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya
hali ya hewa na tabianchi.
Kwa upande wa mratibu wa programu
ya WISER kwa Nchi za Afrika Mashariki, Ndugu. John Mungai alieleza kuwa
lengo la warsha ya uzinduzi huo ni kuwakutanisha wadau na kuwa na uelewa
wa pamoja wa programu hii pia kutoa taarifa ya kuanza kwa utekelezaji
wake kwa wadau wanaohusika katika program hii.
Awali Rais wa TMS Dkt. Burhani
Nyenzi aliwajulisha washiriki kuwa tayari utekelezaji wa awali umeanza
kufanyika kwa kuwajengea uwezo wadau wa sekta husika pamoja na
wanahabari katika mikoa ya Dodoma, Simiyu, Tanga na Manyara.
Programu hii inafadhiliwa na
Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Kimataifa la maendeleo
(DFID) na ulijumuisha wadau mbalimbali wakiwemo wizara na taasisi za
serikali, taasisi zisizo za kiserikali (NGO), mashuleni, watendaji wa
vijiji na wanahabari.
No comments:
Post a Comment