Pages

Thursday, August 1, 2019

TIGO YAIPA MSAADA WA KOMPYUTA 10 SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KISUTU, DAR


 Afisa uwajibikaji kwa jamii wa Tigo , Halima Okash. (kushoto) akimkabidhi mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu , Sylvia Lyimo (wa pili kulia) moja wapo ya kompyuta 10 zilizotolewa na kampuni ya Tigo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam (wa pili kushoto ni Diwani wa kata ya Kisutu Kheri Mohamed Kessy.
Afisa uwajibikaji kwa jamii wa Tigo , Halima Okash. Akionyeshwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu jijini Dar es Salaam,jinsi ya kutumia kompyuta mara baada ya kukabidhi msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa na kampuni ya Tigo, kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sylvia Lyimo. Baadhi ya wanafunzi wakifurahia kutumia kompyuta muda mfupi baada ya kukabidhiwa masada wa komuta 10 kutoka Kampuni ya Tigo. Na Mwandishi Wetu. Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidigitali nchini Tanzania ya Tigo, leo imetoa msaada wa... kompyuta 10 shule ya sekondari ya wasichana Kisutu, pamoja na kuwaunganisha na intaneti ya bure kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata elimu kupitia teknolojia ya kisasa. Msaada huo umeenda sambamba na uzinduzi wa kituo cha kupata elimu kutumia njia za kisasa za kidigitali kwa shule za Sekondari mkoani Dar es Salaam. Wanafunzi watawezeshwa kupata fursa ya kutumia kituo hicho kupata maarifa ya matumizi ya kompyuta na TEHAMA. Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Afisa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo, Halima Okash alisema, “Msaada huu tuliotoa leo kusaidia shule ni moja ya ufanikishaji wa mkakati wetu wa kuwezesha matumizi ya kidigitali ambapo shule zikiwezeshwa kutumia teknolojia kufundisha wanafunzi, wataweza kupata maarifa sambamba na kunufaika kwa kutoachwa nyuma katika mapinduzi ya kiteknolijia ya Kisasa matumizi ya TEHAMA yanayoendelea duniani”. Alisema kutokana na ongezeko la matumizi ya kompyuta nchini Tanzania, sio shule zote zinauwezo wa kutoa elimu ya matumizi ya teknolojia hii. Moja ya changamoto inayowakabili wanafunzi wa shule za sekondari nchini ni kukosekana kwa nyenzo za kuwawezesha kupata elimu inayohusiana na matumizi ya teknolojia za kisasa. “Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu, sasa wanaweza kupata mafunzo ya matumizi ya kompyuta katika mitaala ya masomo yao. Elimu ya TEHAMA inaweza kuleta mabadiliko haraka katika sekta ya elimu, ambapo wanafunzi wanaweza kupata maarifa kutoka kwenye mitandao na tovuti mbalimbali za kielimu, kujifunza mambo mengi na kupata ujuzi unaotakiwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi.” alisema. Aliongeza kusema “Uzinduzi wa kituo hiki cha kutoa elimu kupitia TEHAMA, unadhihirisha dhamira ya kampuni ya Tigo, kufanya uwekezaji katika miradi ya kusaidia jamii hususani kuleta mapinduzi ya sekta ya elimu kuwa ya kisasa na ya kidigitali, sambamba na kufanya shule hii kuvutia wanafunzi wengi wa shule jirani wenye kiu ya kupata elimu ya matumizi ya kompyuta na TEHAMA. Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Kisutu, Mh. Khery Kessy, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi aliipongeza kampuni ya Tigo, kwa juhudi zake za kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya kusomea nchini. “Nawashukuru Tigo kwa msaada huu, kwa kuwa utawezesha wanafunzi kupata maarifa ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa mapema wakiwa bado wako katika madarasa ya chini katika safari yao ndefu ya kutafuta elimu. Ujuzi watakaopata kupitia kompyuta hizi utawawezesha kwenda na wakati wa kisasa na kuweza kuwa na sifa ya kupata ajira.” alisisitiza. Mmoja wa wahitimu wa programu ya Tigo inayojulikana kama Change makers, ya mwaka 2014, amejitolea kushiriki kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo na kushirikisha wanafunzi kutoka shule nyingine za sekondari, ufadhili huu wa kampuni ya Tigo utawezesha wanafunzi kushiriki na kuwavutia kutaka kujua matumizi ya TEHAMA katika kufanikisha ndoto zao katika masomo yao. Katika miaka ya karibuni, kampuni ya Tigo imetoa msaada wa kompyuta 77 katika shule na vyuo vya Serikali, ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma, Shule ya Sekondari ya Jangwani, iliyopo jijini Dar es Salaam, shule 3 za sekondari mkoani Mtwara na shule moja ya msingi mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment