Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM
Serikali kupitia wizara ya afya imepiga hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.
Hayo
yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa
Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati
akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.
Dkt.Kwesi
alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona
namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.
“Tuna
pengo la rasilimali mbalimbali na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao
Mpango kazi wetu na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na
kutakavyosaidiana kutekeleza,” alisema Dkt.Kwesi
Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.
Awali
Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu
wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu
na ulemavu kwa jamii.
“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao”.Alisema Dkt.Subi
Alisema
wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na
hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa
“Wilaya
ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi
iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24
ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na
wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu”.
Naye
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi
Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na
minyoo ya tumbo bado inahitajika kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya
wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na
usubi.
No comments:
Post a Comment