Pages

Wednesday, August 28, 2019

TAFITI SABA ZA MAGONJWA YA MOYO ZILIZOFANYWA NA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUWASILISHWA KATIKA MKUTANO WA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA UNAOTARAJIA KUFANYIKA WIKI IJAYO NCHINI ZAMBIA

Wataalamu wa Afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walifanya tafiti saba za magonjwa ya moyo ambazo zitawasilishwa  katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzielezea tafiti hizo kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo pichani)  kuhusu tafiti saba za magonjwa ya moyo  zilizofanywa na Taasisi hiyo ambazo zitawasilishwa  katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Swai akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo pichani)  kuhusu utafiti wa shinikizo la damu na tatizo la kisukari uliofanywa na Taasisi hiyo  ambao ni moja ya tafiti saba za magonjwa ya moyo  ambazo zitawasilishwa  katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.(Picha na JKCI).

No comments:

Post a Comment