Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe
wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini waliomtembelea Ofisini
kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifafanua jambo alipokutana na Ujumbe
wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini Ofisini kwake Bungeni
Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland
hapa nchini walipokutana na kufanya mazungumzo Ofisini kwake Bungeni
Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)Na Omary Machunda - Bunge
Spika
wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai ameishukuru Serikali ya Ireland kwa
kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya sheria na
haki za binadamu.
Mheshimiwa
Spika ametoa shukrani hizo leo ofisini kwake Bungeni JIjini Dodoma
wakati alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria wa haki za binadamu kutoka
Ubalozi wa Ireland wakiongozwa na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini
Mheshimiwa Bronagh Carr.
Alisema
Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo na Serikali ya Ireland
katika masuala hayo ya sheria pamoja na kudumisha haki za binadamu.
Aidha,
alisema upo umuhimu ujumbe huo, ukakutana na Umoja wa Wabunge Wanawake
nchini (TWPG) ili kujadili changamoto za kijinsia zilizopo katika maeneo
yao na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwa Ireland imepiga hatua kubwa kwenye
masuala ya usawa wa kijinsia.
aliwataka
pia wakutane na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii ambapo miswada yote inayoathiri huduma za jamii ikiwemo masuala ya
elimu na jinsia hujadiliwa kwenye kamati hiyo kabla ya kuingia Bungeni.
“Katika
suala la usawa kwa jinsia Bunge letu limepiga hatua kubwa ambapo
Wabunge wa Viti Maalum Wanawake ni asilimia 30 ya Wabunge wote 393 pia
wapo Wabunge wa majimbo ambao ni Wanawake hivyo kuongeza nafasi ya
uwakilishi wa jinsi hiyo Bungeni” alisema Mheshimwa Spika.
kwa
upande wake Kaimu Balozi wa Ireland, Mheshimiwa Bronagh Carr
alimshukuru Mheshimiwa Spika kwa kukubali kukutana nae pamoja na Kamati
za Bunge.
Alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland umekuwepo kwa kipindi cha miaka 40 na unazidi kuimarika siku hadi siku.
Ujumbe
huo umelenga kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya
kisheria ikiwemo Wabunge, Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali pamoja
na Jeshi la polisi nchini ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya
sheria na jinsia.
No comments:
Post a Comment