Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu
Alibainisha
hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho
ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu.
Alisema
kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na
uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika
kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine.
“Mfumo
huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa
unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo
na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya
mkononi”, alisema Bw. Mabala.
Mwandishi
huyo wa Vitabu ametoa wito kwa wadau, ikiwemo Serikali kuhamasisha
matumizi ya Simu zenye uwezo wa kutumia mfumo wa GePG, hasa katika
maeneo ya vijijini ambako idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wakulima
wanapatikana.
Tanzania
inaidadi kubwa ya vijana ambao wanauwezo wa kutumia mfumo wa
kielektroniki katika malipo ya Serikali ukilinganisha na wazee, hivyo
umekuja wakati mwafaka na utakua na nafasi kubwa ya kuchochea
maendeleleo ya kiuchumi.
Bw.
Mabala amesema kuwa, Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika
Mipango ya Serikali ukilinganisha na awali ambapo mfumo huo haukuwepo
hivyo uwepo wa GePG utaongeza ufanisi kiutendaji na kuharakisha
maendeleo kulingana na ushindani uliopo katika nyanja mbalimbali duniani
hasa katika mifumo ya teknolojia.
Kwa
upande wao wanafunzi wa Sekondari ya Biashara iliyopo Bariadi Mkoani
Simiyu, wameipongeza Serikali kwa kutumia mfumo wa kisasa wa GePG, hivyo
elimu waliyoipata katika maonesho ya Nanenane wataipeleka kwa wazazi
wao na jamii inayowazunguka ili waweze kuitumia katika malipo ya
Serikali.
No comments:
Post a Comment