Mnamo Jumatano, Julai 24, 2019 mtaa wa Kitengela jijini Nairobi nchini Kenya ulikuwa umejawa na furaha tele pamoja na nderemo huku mzungu aliyekuwa amevalia mavazi ya kidini akipita.
Michael Job, mhubiri kutoka Marekani alikuwa amevalia mavazi yake ya kuigiza huku akiwa ameachilia nywele zake.
Nairobi
Karibia waumini wote walikuwa na furaha ya kumuona mwanaume huyo
aliyedhaniwa kuwa ndiye Yesu wa kisasa huku akitembea kwa madaha na
kuzungumza kwa ujasiri mkubwa.
Hata hivyo, licha ya wengi wao kumfahamu kuhusiana na mahubiri yake hakuna aliyekuwa akimtambua zaidi.
Wakati mwingine huvalia mavazi ya kawaida na kupiga picha tu kama watu wengine.
Kwa
mujibu wa picha zake ni ishara tosha kuwa ni mtu ambaye anapenda
kusafiri sana na kukutana na watu kutoka tabaka mbalimbali. Mhubiri huyo
pia huwa na utani.
Japo ulidhania mhubiri huyo hushinda amevalia mavazi yake ya uigizaji basi sio hivyo kulingana na picha zake.
Mugizaji
huyo alikuwa miongoni mwa wahubiri walioalikwa kuidhinisha misa ya
madhehebu mbalimbali ya kikristo kwa jina Kiserian Mega
Interdenominational.
Badala
ya kuendesha punda, alikuwa akitimbelea kwa gari la kifahari akiwa
chini ya ulinzi mkali huku akiwatazama wakazi hao wenye furaha akiwa juu
ya gari.
Bado baadhi ya watu wamesalia na maswali ya mbona mhubiri huyo alikuwa akisisitiza kuitwa ' Yesu Kristu wa kisasa.
No comments:
Post a Comment