Pages

Thursday, August 1, 2019

MAONESHO YA NANENANE NYAKABINDI SIMIYU: RC ANTHONY MTAKA AIPONGEZA WCF


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel kwenye viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Simiyu.
Mhe. Mtaka akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la WCF
 Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtaka, akiongozana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence baada ya kutembelea banda la Mfuko huo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa  Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (kulia), akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la WCF.

Afisa Matekelezo Mwandamizi (WCF), Bw. Musa Mwambujule (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyetembelea banda namba 13 la WCF kwenye viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu leo Agosti 1, 2019.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa  Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia), akitoa elimu kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa huo kuanzisha kiwanda cha vifaa tiba kwa kutumia malighafi ya pamba.
Mhe. Mtaka ametoa pongezi hizo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu wakati alipotembelea banda la WCF linaloshiriki maonesho ya Nanenane. mwaka  2019.
“Mimi kama kiongozi wa serikali ya Mkoa, ninawashukuru sana WCF kama partner (washirika) wakubwa sana kwenye mkoa wetu hususan kwenye ujenzi wa kiwanda cha vifaa tiba.” Alifafanua.
Alisema WCF kupitia Mkurugenzi Mkuu wake, Bw. Masha Mshomba na wakurugenzi wengine wamekuwa wakishirika wakubwa katika vikao vingi vya mkoa vinavyohitaji washirika (partners).
Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari site clearance imefanyika na wizara inaelekea kutangaza zabuni ili mradi uanze kutekelezwa.
Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi yamefunguliwa rasmi leo Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.”
Akizungumzia ushiriki wa WCF kwenye maonesho hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anselim Peter amesema, maonesho hayo ni fursa nzuri kwa Mfuko kuelimisha waajiri, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko.
“Tupo hapa ili kutoa elimu kwa wafanyakazi, elimu kwa waajiri namna gani wanaweza kuwasilisha madai yao pale mfanyakazi anapopata madhara kutokana na kazi ili hatimaye aweze kupata fidia stahiki na kwa wakati.” Alisema.
Amewakaribisha wananchi wakiwemo waajiri kutoka Simiyu na mikoa jirani ya Shinyanga na Mara kufika kwenye banda la WCF namba 13 lililo jirani na lango kuu la kuingia viwanja vya Nyakabindi ili kupata elimu zaidi kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na WCF.
“Katika banda letu, tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za waajiri kujisajili na Mfuko, kwani tunatambua Mkoa wa Simiyu unakuja juu katika uwekezaji wa viwanda kwahivyo tunategemea waajiri wapya wengi kutoka hapa.” Alisema.

No comments:

Post a Comment