WAKAZI
wa Kisarawe wamenufaika na kambi ya kwanza ya kampeni ya uchunguzi na
matibabu dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza inayotolewa na madaktari
bingwa wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma China (DCAT).
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Seleman Jafo akiwashukuru wanajumuiya ya Watanzania
walioishi nchini China (DCAT) kwa kujitolea kuwapa huduma ya afya bure
kwa wakazi wa wila ya Kisarawe, Pwani.
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (kushoto) akimkaribisha Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Seleman Jafo kutoa hotuba yake.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate
Mwegelo amesema utoaji wa huduma bora za afya ni miongoni kwa
vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli
na kwamba msisitizo zaidi ni katika utoaji wa huduma za kinga.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma nchini China Dkt. Liggyle
Vumilia akielezea kwa ufasaha huduma hiyo ya afya bure.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Utamaduni wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Bwana Gao Wei akisoma hotuba yake.
Mtaalam wa Tiba ya jadi ya Kichina Dkt Paul Mhame akitoa ushauri kwa jamii.
Wananchi
wa wilaya ya Kisarawe, Pwani na vitongoji vyake wakipima uzito na urefu
ili kuweza kupatiwa matibabu ya bure kutoka kwa Jumuiya ya Madaktari
Bingwa Watanzania waliosoma nchini China (DCAT) waliopiga kambi kwa muda
wa siku tatu. Jumuiya hiyo imejipanga kuendelea na zoezi la kutoa
huduma katika mkoa wa Tanga na maeneo mengine ya Tanzania. Picha na
Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza akitoa maelekezo kwa wagonjwa.
Wagonjwa wakipimwa presha.
Wagonjwa wakipimwa ugonjwa wa Kisukari.
Mtatibu wa zoezi la upimaji wa Afya Bure, Bi. Linas akigawa maji kwa wagonjwa.
Dokta Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Dkt Heri Tungaraza akitoa maelekezo kwa wagonjwa.
Wagonjwa wakipimwa presha.
Wagonjwa wakipimwa ugonjwa wa Kisukari.
Mtatibu wa zoezi la upimaji wa Afya Bure, Bi. Linas akigawa maji kwa wagonjwa.
Wananchi wakisubiri huduma.
Wazee
wakipatiwa ushauri kabla ya kuingia kuwaona Madaktari bingwa
waliojitolea kufanya zoezi la kutoa huduma ya Afya Bure kwa wananchi wa
Jumuiya ya Madaktari Bingwa Watanzania waliosoma nchini China (DCAT).
Kila mmoja alijitahidi kumleta mgonjwa wake ili apatiwe huduma ya afya bure.
Wananchi
wa wilaya ya Kisarawe, Pwani na vitongoji vyake wakipimwa presha ili
kuweza kupatiwa matibabu ya bure kutoka kwa Jumuiya ya Madaktari Bingwa
Watanzania waliosoma nchini China (DCAT) waliopiga kambi kwa muda wa
siku tatu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma nchini China Dkt. Liggyle
Vumilia (aliyevaa tai) akitoa ushari kwa wagonjwa walifika kupatiwa
huduma ya Afya bure iliyofannyika wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Wananchi wa wilaya ya Kisarawe wakiwa wamepanga foleni kuoatiwa huduma ya Afya Bure.
Watoa huduma wakiendelea kutoa ushari kwa wagonjwa waliofika kupatiwa huduma ya Afya bure.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Watanzania waliosoma nchini China Dkt. Liggyle Vumilia akigawa maji kwa wagonjwa aliojitokeza kupatiwa huduma ya Afya Bure.
Awali
akifungua kambi hiyo wiki hii katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Seleman Jafo amewahamasisha kujitokeza kwa wingi ili kujua
hali zao.
Jafo
ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe ametumia fursa hiyo kuwasilisha ombi
lake kwa Mwambata wa Ubalozi wa China, anayeshughulikia masuala ya
utamaduni na elimu, Gao Wei, ambaye alimwakilisha Balozi wa China,
kwamba waijengee Hospitali hiyo jengo la kisasa la matibabu.
"Tunashukuru
wataalamu wetu wameona katika kampeni hii, Kisarawe iwe ya kwanza kisha
watakwenda maeneo mengine ya nchi, Rais Dk. John Magufuli anatujengea
jengo la kisasa la OPD (wagonjwa wa nje) hapa Kisarawe.
"Nitumie
fursa hii kuuomba ubalozi wa China, ikizingatiwa pia kwamba Wilaya hii
ina historia hasa katika ujenzi wa reli ya Tazara, Wachina walikaa hapa
na wakazi wa Kisarawe walishiriki kuijenga.
"Ukiacha
mahusiano yale ya ujenzi wa reli ya Tazara, leo hii wigo umepanuka
mpaka kwenye elimu, afya na sekta nyinginezo," amesema.
Ameongeza
"Nawasihi wakazi wa Kisarawe kuitumia fursa hii ya uchunguzi vizuri,
hata yule mwenye mgonjwa aliyepo nyumbani amlete, hapa Wapo madaktari
wabobezi watachunguzwa na watagundua tatizo linalomsumbua.
Kuhusu
ombi hilo la Waziri Jafo, Mwambata huyo wa Ubalozi amesema amelipokea
na kuridhia kwamba wapo tayari kujenga jengo la kisasa kwa Hospitali
hiyo.
Awali,
amesema ushirikiano wa China na Tanzania ni wa miaka mingi na imekuwa
ikitoa ufadhili kwa watanzania kwenda kusoma nchini humo elimu
mbalimbali .
Amesema wanafurahi kuona kwamba wataalamu waliopata ufadhili wa masomo China sasa wanasaidia nchi katika mambo mbalimbali.
Mwenyekiti
wa DCAT, Dk. Liggyle Vumilia amesema katika siku hizo tatu wanatarajia
kuwachunguza afya watu kati ya 600 hadi 1000 ambapo watachunguzwa
magonjwa ya saratani, moyo, kisukari na mengineyo.
"Kampeni
yetu ina kauli mbiu 'Jali Afya yako, Fanya uchunguzi mapema', tunalenga
wananchi wa kawaida kabisa, kuwahamasisha wajenge tabia ya kuchunguza
afya zao, itawasaidia kujua mapema kama wanakabiliwa na matatizo au la!
"Wale
tutakaowakuta na matatizo madogo tutawatibu kupitia mfuko tulioandaa,
tunawapa na elimu ya kujikinga dhidi ya magonjwa haya," amesema.
Amesema wanatarajia pia kwenda hivi karibuni mkoani Tanga ambako watafanya kampeni hiyo na baadae nchi nzima.
Mkuu
wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo amesema utoaji wa huduma bora za afya ni
miongoni kwa vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais Magufuli na kwamba msisitizo zaidi ni katika utoaji wa huduma za
kinga.
No comments:
Post a Comment