BARA la Afrika lina nafasi kubwa
ya kupambana na umaskini na vikwazo vinavyozuia kuyafikia maendeleo na
hiyo ni kutokana na kizazi cha sasa kuwa kizazi cha kwanza kabisa kuishi
katika bara hilo wakishuhudia ukuaji wa uchumi ukifikia asilimia 4 kwa
nchi nyingi barani humo.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya The
African Wildlife Kadu Sebunya amesema kuwa bara la Afrika tangu mwaka
1994 limeshuhudia vipindi virefu ya ukuaji wa kiuchumi tangu kipindi cha
ukoloni katika miaka ya
sitini, lakini bara la Afrika limeendelea kukua
na kubadilisha fikra pamoja na kuyabadilisha mataifa mengi ya Afrika
kwa kuwa na uchumi unaojitegemea na unaokua kwa kasi ulimwenguni.
Amesema kuwa uwekezaji katika
tafiti, uvumbuzi, elimu, na huduma za afya umeendelea kupunguza kasi ya
kuenea kwa magonjwa pamoja na kuongeza kasi ya kujiandikisha shule
ambapo mamilioni ya watoto wanajiandikisha mashuleni kupata maarifa
licha ya bara hilo kutokuwa katika nafasi nzuri katika masuala ya
kisiasa.
Aidha amesema kuwa “Maendeleo ni
Kuchagua” na hiyo itafanikiwa ikiwa viongozi wa Afrika na washirika wa
maendeleo katika ngazi zote watapambana dhidi ya changamoto
zinazozikumba nchi husika ikiwemo uchimbaji wa rasilimali, miundombinu
hafifu, kilimo kisicho faafu, uharibifu wa mito, nyasi, mbuga za wanyama
na misitu; vitu ambavyo wananchi wanavitegemea na hugharimu maendeleo.
Kadu amesema kuwa bara la Afrika
ni mboni ya uhifadhi wa maliasili pamoja na viumbe wakiwemo robo tatu ya
spishi za mamalia duniani wapatao 4700, ndege 2000,aina 2000 za samaki,
na amfibia spishi 950 na hiyo ni pamoja na maelfu ya mimea yenye
thamani pamoja na wanyama wa mwituni ambao wanawakilisha uasilia, uchumi
na ikolojia.
Utajiri wa Bara hilo umeelezwa
zaidi hasa katika sekta za mafuta na gesi asilia na hiyo ni pamoja na
kuwa na kampuni zenye umiliki wa hifadhi ya madini wa asilimia 40
duniani licha ya mlengo wa majadiliano ya sasa kuhusiana na maendeleo
Afrika yameegemea zaidi katika unyonyanyi wa rasilimali na namna bora ya
kuyafikia maendeleo.
Imeelezwa kuwa bara la Afrika ina
maelfu ya utajiri katika sekta za utalii, madini na gesi na kwa sasa
kinachotakiwa ni kuangaza macho katika mambo ya msingi ikiwemo madini,
miundombinu, mafuta na gesi asilia, kilimo, makazi na mifumo ya wanyama
kutegemeana pamoja na usimamizi endelevu wa rasilimali zake asili za
kiafrika, mazingira, wanyama pori pamoja na ardhi.
Kupitia mkutano huo Kadu
amewashukuru watoa mada wa mkutano huo akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya
tatu Rais Benjamin Willium Mkapa na Rais Mogae kwa kushirikiana na
taasisi hiyo katika msingi wa wanyamapori wa kiafrika na katika mada zao
wamesisitiza mambo muhimu sana kuhusiana mazingira, wanyamapori, na
maeneo ya porini na kueleza kufikia mwaka 2063 Afrika litakua bara la
maendeleo lenye kutumia rasilimali zake kukiletea maendeleo na
kuyasimamia.
No comments:
Post a Comment