NAIBU WAZIRI WA AFYA WA CHINA MHE. LIN BIN ATEMBELEA JKCI KUONA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO WANAZOZITOA
Daktari
bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akiwaelezea Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri
wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin jinsi wauguzi wa
chumba hicho wanavyowahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu
Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin
wakimsikiliza mtoto anayetibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara iliyofanywa na Naibu
waziri huyo ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya
Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma
timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya kambi maalum
ya upasuaji wa moyo.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akimwelezea Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe.
Lin Bin namna ambavyo chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa watoto wenye
magonjwa ya moyo kitakavyorahisisha huduma za matibabu katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo alitembelea JKCI leo kwa
ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi
hiyo.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin
wakizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) wakati wa ziara fupi ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo
zinayotolewa na Taasisi hiyo. Naibu Waziri huyo alitembelea kambi maalum ya
upasuaji wa moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa
China na kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo
na matibabu ya moyo baina ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na Hospitali kuu ya
jimbo la Shandong.
Naibu
Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin akimpa pole
mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya
matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali
ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili
ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu
Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li Leping wakisaini mkataba wa makubaliano ya
kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo
jijini Dar es Salaam. Moja ya makubaliano hayo ni
wataalamu wa afya kutoka JKCI kwenda katika hospitali hiyo kujifunza matibabu
ya moyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu
Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandongla nchini ChinaLi Leping wakibadilishana
mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina
ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo
kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo
wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya
Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa
JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo
wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya
Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa
JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya
watu wa China Mhe. Lin Bin wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hospitali
ya jimbo kuu la Shandong na Ubalozi wa
China nchini wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. (PICHA
NA GENOFEVA MATEMU – JKCI)
No comments:
Post a Comment