Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika ziara ya kukagua kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Mkuranga Pwani. |
Meneja
Uzalishaji Bw. Nurdin Bofu akimuonesha jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki wakati wa ziara yake
katika kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza Jasi (Gypsum
Board) cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa lengo la
kukagua mazingira ya wawekezaji wa kiwanda hicho kwa nia ya kuendelea
kuboresha mazingira yao ziara ilifanyika Juni 28, 2019.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akihutubia washiriki wa mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda cha KNAUF ili
kuzungumza nao masuala ya uboreshaji wa mazingira ya wawekezaji nchini
wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
akiangalia moja ya malighali zinazotumika katika kiwanda cha KNAUF
(Metal Profile) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda
hicho na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipata
maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara
kuhusu namna wanavyopakia unga maalumu wa kutengeneza jasi wakati wa
ujenzi wakati wa ziara yake.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
akiangalai moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda kinachotengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Meneja
Fedha wa kiwanda cha KNAUF akiwasilisha hotuba kuhusu kiwanda hicho
wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.
Angellah Kairuki kiwandani
|
Meneja
wa Mradi kutoka kiwanda cha KNAUF Bw. Norbert Wagner akimuonesha
michoro ya ramani ya kiwanda hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea na kukagua mazingira yao
Juni 28, 2019.
hapo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)NA MWANDISHI WETU – OWM
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.
Angellah Kairuka ameutaka uongozi wa kiwanda kinachotengeneza bidhaa za
cha za jasi (Gypsumboard) cha KNAUF kuendelea kushirikiana na jamii inayowazunguka katika kujiletee maendeleo.
Ametoa
kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii alipotembelea kiwanda hicho
kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili
kukagua shughuli za uzalishaji zinazoendela pamoja na kusikiliza
changamoto za wawekezaji hao na kuweza kujadili masuala ya kuendelea
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Waziri
Kairuki aliwataka kuona umuhimu wa kuchangia katika shughuli za
kimaendeleo katika maeneo yanayozunguka kiwanda hicho hususan katika
uboreshaji wa miundombinu na utoaji wa misaada itakayofikia jamii kwa
sehemu kubwa na si mtu mmoja mmoja ili kuleta maendeleo katika eneo
kubwa na kuondoa tofauti kubwa za kimaendeleo zisizoendana na maendeleo
ya maeneo kiwanda hicho.
“Ni
muhimu sana, na ni busara kuona ni kwa namna gani mnashirikiana na
wananchi wanaozunguka eneo hili katika kuleta maendeleo ili kuhakikisha
mnakubalika , na kuleta maendeleo ya eneo husika na kuondoa tofauti za
kimaendeleo kati ya ustawi wa kiwanda na jamii inayowazunguka”alieleza
Waziri Kairuki
Waziri
aliutaka uongozi huo kushiriki kimalilifu katika shughuli za maendeleo
ikiwemo kuchangia kuboresha miundombinu inayozunguka mazingira ya
kiwanda ili kuendelea kushiriki kwa vitendo na kuunga mkono jitihada za
kuendelea eneo hilo.
Sambamba
na hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jumaa Abeld
aliomba uongozi wa kiwanda kuona namna ya kuchangia katika maendeleo ya
eneo lao kwa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa sita katika shule
ya msingi ya Kitangwi pamoja na madarasa manne katika shule ya msingi
ya Kisemvule zilizopo Wialya ya Mkuranga katika mkoa huo.
“Ombi
letu ni kuona namna kiwanda hiki kinavyoweza kuchangia katika maendeleo
kwa kutujengea vyumba sita vya madarasa katika shule zinazotuzunguka
ili kusaidia uhaba uliopo na kusaidi watoto wetu kujifunza katika
mazingira mazuri,”alisema Jumaa.
Aidha
Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara aliahidi ifikapo
Julai 05 mwaka huu uongozi wa kiwanda utatoa taarifa za utekelezaji wa
maombi hayo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 6.
“Tunaahidi
kukutana kama uongozi wa kiwanda ili kujadili na kutekeleza masuala ya
msingi ikiwemo hili la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuendelea
kuleta tija kwa uwepo wa kiwanda katika eneo hili,”alisema Mwasara.
Naye,
Meneja Fedha wa kiwanda hicho Bi. Wema Mboga alishukuru Serikali kwa
kuendelea kuboresha mazingira ya wawekezaji nchini na kumpongeza ziara
ya Waziri katika kutatua na kuahidi kufanyia kazi masuala yaliyoelezwa
kuwa ni changamoto kiwandani hapo ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa
nishati ya umeme ya uhakika, kutokamili kwa leseni za uchimbaji kwa
wakati, tozo kubwa za malighafi na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji
kiwandani hapo.
AWALI
Kiwanda cha KNAUF kilianzishwa mwezi Novemba mwaka 2015 kwa lengo la kuzalisha bidhaa za jasi (Gypsum board), gundi za jasi, pamoja na chuma za jasi (metal profile) kufanya
kazi na usambazaj.Kiwanda kinafanya kazi katika nchi zaidi ya 80 ambapo
katika nchi za kusini mwa Janga la Sahara, Tanzania ni nchi pekee
ambayo ina uwekezaji huo kutokana na sababu za mazingira mazuri ya
kibiashara na uwekezaji pamoja na sababu za kijiografia.Kampuni imeajiri
wazawa 150 katika Nyanja zote kwa kulenga ifikapo 2020 kiwanda kiweze
kuendeshwa na wazawa pasipo kutegemea wataalam kutoka nje.
No comments:
Post a Comment