Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania imeendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa
mfumo wa alama za vidole ikishirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya
Taifa (NIDA) Jeshi la Polisi Kitengo cha makosa ya mtandaoni,Uhamiaji
pamoja na watoa huduma za mawasiliano, stendi kuu ya mabasi mjini Moshi
Mkoani Kilimanjaro.
Mabel
Masasi ni Afisa mwandamizi wa habari na mahusiano kutoka TCRA ambapo
amesema kuwa Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu juu ya
matumizisahihi ya vifaa vya mawasiliano,ambapo NIDA wanawasaidia
wananchi kupata vitambulisho vya Taifa ambapo mzunguko huo umekuwa
ukifanyika nchi nzima ambapo Kilimanjaro ni mkoawa 10.
Amesema
kuwa wataendelea kuzunguka mikoa yote lengo kuu likiwa ni kufanya
uhamasishaji wa kusajili kwa namba za vitambulisho vya Taifa na kwa
alama za vidole na ili kurahisisha huduma kwa wananchi ambao
wamejitokeza katika zoezi hilo.
Masasi
amesema kuwa zipo changamoto malimbali walizokutana nazo na wamejaribu
kuyatatua kadiri wanavyozidi kwenda mikoani,amesema kubwa zaidi ni vile
amabavyo wananchi wengi wamekuwa wakilalamika hawazijui namba zao za
vitambulksho ambapo tumewasihi NIDA waweze kutatua changamoto hiyo kwa
wananchi.
Calistus
Mhode ni Mkaguzi maidizi kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha makosa ya
mtandaoni amesema amesema zoezi hilo linaendelea nchi nzima la mnada kwa
mnada ambapo wanashirikiana na Taasisi nyingine za serikali katika
kuielimisha jamii na kuwafikia wananchi juu ya matumizi sahihi ya
mitandao ya kijamii,na matumizi ya teknolojia kwa ujumla .
"Tunawataka
wananchi wote wanaokuwa na changamoto zakipolisi sisi tupo tayari
kuwaelimisha na kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali amabazo
zimewakumba "alisema Calistus.
Abubakari
Kakinga Afisa wa NIDA mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa wataendelea
kutoa hudumakwa wananchi na kama vitambulisho vitakuwa vimechelewa
wananchi wanawezakutumia namba za vitambulisho vyao kupata huduma
malimbali kama usaajili wa simu zao.
Amewahimiza
wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kujisajili ya kupata
kitambulisho cha Taifa wasisubirie hadi pale zoezi litakapofungwa.
No comments:
Post a Comment