Mkurugenzi
Msaidizi
wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula, Bwana Beatus
Malema, akiwa na Meneja Mkuu wa We Farm, Bw. Nicholaus John (kulia) na
Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Wakulima cha taasisi ya We Farm,
Bi.CyrilaAnthony, akizinduan huduma hiyo kwa kugusa nembo (logo) ya
taasisi hiyo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Juni 28,
2019.
Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Wakulima cha taasisi ya We Farm, Bi.CyrilaAnthony, akitoa hotuba yake. |
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
TAASISI ya tunalima WE FARM imezindua mfumo wa kuwawezesha wakulima kubadilishana taarifa kwa kutuma ujumbe mfupi
kupitia simu za kiganjani.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2019, Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula, Bwana Beatus Malema
amesema, mfumo huo utawezesha kusaidia njia inayotumiwa kwa sasa ya kuwaelimisha
wakulima kwa kutumia Maafisa ugani.
“Mfumo
huu lengo lake ni kutengeneza mtandao wa mawasiliano na utawezesha wakulima
kuweza kutuma ujumbe wowote ili kuuliza chochote kuhusu shamba lake au katika
eneo lake la kazi na majibu yatatolewa papo hapo.” Alifafanua Bw. Malema.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu wa WE FARM , Bw.Nicholaus John alisema huduma hiyo ni bure na mkulima atatuma
ujumbe mfupi kupitia namba 15088.
“Mkulima
ataweza kuuliza maswali na kupata majibu kutokana na matatizo mbalimbali
yaliyopo shambani wkake, wazo hili lilikuja kutokana na kwamba wakulima
wanachangamoto nyinginmashambani lakini wanakosa habari au ujuzi wa kuweza
utatua matatizo yao.” Alisema na kuongeza….Kinachofanywa na WE FARM ni
kumuwezesha mkulima kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa wakulima wenzake
na hivyo kumuwezesha kuendelea na kilimo chake kwa njia iliyo sahihi.” Alisema
No comments:
Post a Comment