Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika
kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, uliofanyika
Tuwavushe Salama, Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka( wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi na wadau wa afya baada ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji
katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE,
Tuwavushe Salama, uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani
Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo
pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia
vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama,
uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina
Begum na Mratibu wa UNFPA Mkoa wa Simiyu, Dt. Amir Batenga wakiteta
jambo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika
kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe
Salama, uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa
nchini, DKT. Hashina Begum akizungumza na viongozi na wadau wa afya
Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika
kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe
Salama, uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani
Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo
pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia
vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama,
uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Dinna Atinda akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani
Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia vifo
vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama,
uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mageda Kihulya
akiwasilisha taarifa ya hali ya vifo vya wanawake na watoto, wakati wa
hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia vifo
vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama,
uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa
Serikali mkoani hapa kuona
umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wa dini, siasa na wa kimila katika
utoaji wa elimu kwa jamii na kuwahamasisha wanawake wajawazito
kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za
afya ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi..
Mtaka ameyasema hayo wakati wa
Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na
uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama uliofanyika Mei 02,
2019 Mjini Bariadi.
“ Ni vizuri tukaongeza wigo wa kutoa elimu
kwa jamii kuhusu umuhimu wa mama wajawazito kuhudhuria kliniki kipindi
cha ujauzito na kuhakiksha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya; viongozi wa dini,siasa na wa kimila wana nafasi kubwa
kwenye jambo hili muone namna ya kuwashirikisha “ alisema Mtaka.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa afya ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) imeboresha vituo vya
kutolea huduma, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia
huduma za afya ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Katika hatua nyingine Mtaka ameishukuru
UNFPA kwa namna ilivyosaidia katika ujenzi wa miundombinu ya afya,vifaa
na vitendea kazi kama magari ya kubeba wagonjwa huku akisisitiza
viongozi na watendaji walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni hii kutoka
na dhamira ya kuwavusha salama akina mama wajawazito na watoto na
kupinga vifo vitokanavyo na uzazi..
Mwakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Dinna Atinda ameusisitiza uongozi wa mkoa
kusimamia vituo vinavyotoa huduma za afya za msingi na dharura
kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa wananchi.
Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Salome Mwijuma ametoa
wito kwa jamii kuendelea kuwasaidia wanawake wajawazito waweze
kuhudhuria kliniki muda wote, wapate lishe bora na kujifungulia katika
vituo vya kutolea huduma ili wajifungue salama.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Mageda
Kihulya amesema mwaka 2015 watoto 680 walifariki na mwaka 2018 watoto
640 walifariki, wakati kwa upande wa akina mama wanaojifungua vifo
vimepungua kutoka 48 mwaka 2015 na kufikia 40 mwaka 2018, jambo ambalo
linaonesha kuwa nguvu ya ziada kutoka wadau mbalimbali inahitajika
kumaliza tatizo hili.
Dkt. Mageda amesema sababu zinazosababisha
vifo vingi vya akina mama wajawazito kama vile kutokwa na damu nyingi
wakati wa kujifungua na mkingamo wa uzazi zinaweza kuzuilika, hivyo
akatoa wito kwa wakina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma
kuzuia vifo hivyo, huku akisisitiza watoto chini ya miaka mitano nao
wapewe chanjo kuzuia vifo..
Makamu Mwakilishi mkaazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa
nchini, Dkt. Hashina Begum amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana
na Serikali katika jitihada mbalimbali za kupunguza vifo vya akina mama
wajawazito na watoto
No comments:
Post a Comment