Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akionesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama
wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania baada ya kuizindua
jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka
Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu
Serikali Dkt Albina Chuwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama
wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo
tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex
David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina
Chuwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi wakati wa
uzindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa
Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo tarehe
3 Mei 2019. Wa pili kushoto waliokaa ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya
Prindex David Ameyaw na wa pili kulia waliokaa ni Mtakwimu Mkuu
Serikali Dkt Albina Chuwa.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, DODOMA
Tanzania
imeshika nafasi ya nne kati ya nchi tisa za Kusini na... Mashariki mwa
Afrika zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa na asilimia 64 ya watu wanaoamini
kuwa hali ya umiliki wa ardhi na makazi ni salama.
Hayo
yalibainika leo tarehe 3 Mei 2019 wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya
Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa
Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Akizungumza
wakati wa kuzindua Ripoti hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kiwango hicho ni kikubwa
zaidi ya wastani wa asilimia 61 kwa nchi tisa zilizofanyiwa utafiti
katika Afrika ya Magharibi.
Aidha, Utafiti wa Ripoti hiyo unaonesha Tanzania
imeshika nafasi ya kumi kati ya nchi 33 zilizoshiriki katika Utafiti
huo kwa kuwa na asilimia zaidi ya hamsini ya watu wanaomiliki makazi yao
wenyewe.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, matokeo ya
utafiti huo yametokana na hatua mbalimbali ambazo serikali imeendelea
kuzichukua ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na usalama wa umiliki
wa ardhi na makazi.
Kawa
mujibu wa Dkt Mabula, kama ungefanyika utafiti mwingine leo basi
huenda matokeo yake yangekuwa tofauti kutokana na Serikali kudhamiria
kupanga , kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi na kutolea
mfano katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali ilipanga kupima na
kumilikisha vipande vya ardhi.
Dkt
Mabula alibainisha kuwa, takwimu zinaonesha kati ya mwezi Agosti 2018
na Machi 2019 Hatimiliki 36,428 zimeandaliwa kwa wamiliki wa viwanja na
mashamba na Hatimili za kimila 286472 ziliandaliwa kwa ajili ya wamiliki
wa ardhi walioko vijijini.
Dkt
Mabula alisema, hatua nyingine ambazo serikali imechukua ni pamoja na
kuanza kutumia mifumo ya kielektroniki katika utoaji huduma za
ardhi ambapo Mfumo Unganishi wa Kumbukumbu za Sekta ya Ardhi (ILMIS)
umeendelea kufanyiwa majaribio katika wilaya za Ubungo na Kinondoni na
kusisistizia kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya umilikishaji
ardhi na kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa..
Kwa
upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dkt Albina Chuwa alisema utafiti uliofanyika ulishirikisha sekta zote
muhimu na kuzitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Global
Land Allience, DFID sambamba na wananchi wote wakiwemo wakuu wa kaya za
Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema,
Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa ripoti yake mwenyewe kati ya nchi 33
na ripoti hiyo itatumiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi katika kupanga mipango yake na kuzitaka taasisi za vyuo kutumia
ripoti hiyo kufanyia utafiti ili kuisaidia sekta ya Ardhi.
No comments:
Post a Comment