Pages

Monday, May 27, 2019

SERIKALI KUJENGA VIWANDA VYA KUSINDIKA MAZAO YA UVUVI NCHINI



Serikali inatarajia kujenga viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi nchini kupitia Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Mei 27 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Katika swali lake Kubenea, lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalumu, Tunza Malapo (Chadema), alihoji ni lini na ni wapi Kiwanda cha Samaki cha Pwani kitajengwa hapo.

No comments:

Post a Comment